• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Tiba asili

Tiba asili

Na MARGARET MAINA

[email protected]

WAZEE wazee wetu wa zamani walitumia sana tiba asili.

Kuna mimea na mazao yanayotokana na miti mbali mbali yenye viungo ambavyo ni dawa. Baadhi ya tiba hizi za nyumbani unazoweza kuzitegema ni kama vile:

Pilipili

Pilipili ina kiungo ambacho kina umuhimu mkubwa wa tiba tangu jadi na sasa matumizi yake yameanza kukubalika na wengi sio tu kupitia chakula lakini pia kama dawa.

Ina kiungo kijulikanacho kama capsaicin ambacho kinatumiwa kudhibiti maumivu ama uchungu. Inafanya kazi kwa kuwasha sehemu ya ngozi kwa kuipa joto na ukali kabla ya kufisha ganzi baadaye.

Tangawizi kutibu maumivu na kichefuchefu

Ni kama ada kutumia tangawizi ukijipata na mafua au koo lako likiwa linakoroma. Tiba hii inafanya kazi na ina uwezo mkubwa sana wa kukupa afueni.

Pia chai ya tangawizi itakusaidia kuzuia kuhisi kichefuchefu. Ili kuitengeza dawa ya tangawizi, unachohitaji ni kuiponda ama kuitumia iliyosagwa na ikakorogwa ndani ya chai.

Tangawizi pia ina viungo vya kutuliza maumivu na mara nyingi hata dawa za homa na mafua huwa zimetengenezwa kwa baadhi ya viungo vya tangawizi.

Mafuta ya mikalatusi

Mafuta ya mikalatusi yana kiungo ambacho hupunguza uchungu.

Kiungo hicho kina athari kama ya morphine na kina uwezo mkubwa wa kukupa afueni unapohisi maumivu.

Hata hivyo matumizi ya mafuta ya mikalatusi sio ya kila mtu kwa sababu mafuta haya yanaweza kuchochea pumu yaani Asthma na pia kudhuru wanyama wa nyumbani.

Lavender

Maumivu ya kichwa wakati mwingine yanaweza kukuathiri ghafla bila kuwa na dawa za kupunguza makali yake.

Iwapo utakumbwa na maumivu haya basi unaweza kutumia lavender au majani yake.

Pia tiba hii ya nyumbani husaidia kupunguza uchovu na matatizo ya kifikira endapo umechoka kupindukia.

Majani ya mnaa

Mnaa unajulikana na wengi na una manufaa mengi ikiwemo kufungua mkondo wa kupumua iwapo umesakamwa au hata kupunguza maumivu ya misuli.

Ukihisi uchungu kwenye misuli, tafuta majani ya mnaa.

Aina nyingine ya mnaa inayotumika sana ni peppermint. Kiungo hiki kinatumika sana kutibu maradhi ya koo au kutoa afueni wakati unakabwa na mafua.

Kando na matatizo ya tumbo, mafuta ya peppermint au chai ya peppermint inaweza kusaidia kupunguza maumivu ya kichwa.

Vyakula vyenye magnesium

Iwapo kuna kiungo kinachoweza kukupa afueni ya matatizo mengi nyumbani basi ni vyakula vyote vyenye madini ya magnesium.

Iwapo utapatwa na matatizo kama uchovu, kuumwa na kichwa na maumivu ya misuli basi tiba hii ya nyumbani itakupa afueni.

Mboga na matunda yenye magnesium ni kama spinachi, parachichi, na hata chokoleti nyeusi.

You can share this post!

Familia ya Tob Cohen haitaki aliyekuwa mkewe akijitambua...

Himizo wakulima wazalishe mazao salama kuwahi soko la...

T L