• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
TIM WANYONYI SUPER CUP: Leads United yamaliza ubishi kwa wapinzani wao

TIM WANYONYI SUPER CUP: Leads United yamaliza ubishi kwa wapinzani wao

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Leads United ni miongoni mwa vikosi vilivyokuwa vikishiriki mechi zilizokuwa zikiandaliwa na Extremes Sports chini ya afisa wake mkuu, Hussein Mohamed.

Mwaka 2019 Extreme Sports ilitangaza kusitisha ligi zote kutokana na changamoto za kupata wadhamini baada ya shirika la kubeti la SportPesa kusimamisha kufadhili sekta ya michezo nchini.

Afisa mkuu wa klabu hiyo, Patrick Lumumba amesema hayo muda tu baada ya kutawazwa mabingwa wapya katika mashindano ya Tim Wanyonyi Super Cup mwaka huu. Leads chini ya nahodha, Kevin Juma ilibeba kombe la taji hilo kwa kuzoa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wapinzani wao Leverkusen FC baada ya kutoka nguvu sawa bao 1-1 katika muda wa kawaida.

”Kwanza sina shaka kutaja kuwa tumepania kurejea kushiriki mechi za ligi lakini hatujaamua ni ligi gani maana yapo masuala tunaojadiliana,” alisema na kupongeza wachana nyavu wake kwa kazi nzuri waliotenda kwenye ngarambe hiyo.

”Buda umeamini. Nakumbuka vizuri sana nilikwambia timu yangu ndio itakayobeba taji la mwaka huu,” kocha wake Wiston Issah alisema na kuongeza kwamba licha ya wapinzani wao kuwapia breki walikuwa wamepangwa kikosi chao vizuri na tayari kufanya kweli.

Katika robo fainali Leads United ililaza City Park B FC goli 1-0, WYSA ilituzwa ushindi wa mezani baada ya wapinzani wao Dimba Patriots kutofika uwanjani kucheza mchuno huo. Nao wanasoka wa White Eagles walifunga Kibagare Sportiff mabao 4-2 kupitia mipigo ya matuta baada ya kutoka sare tasa.

Nao wachezaji wa Simba United walikubali kulala kwa mabao 4-1 mbele ya Leverkusen FC magoli 4-1.

Timu ya Leads United ambayo imefanikiwa kubeba ubingwa wa taji la Tim Wanyonyi Super Super 2020. Picha/John Kimwere

KULEA

Timu hiyo inajivunia kuwa miongoni mwa timu ambazo zimefanikiwa kukuza wachezaji wachache waliobahatika kujiunga na klabu za hadhi ya nchini. Baadhi ya vijana hao wakiwa Nahashon Alembi (KCB), Mark Otieno (Wazito) na Kevin Alilo (AFC Leopards).

Leads United inashirikisha: Isaiah Wakasala, Ochieng Erick, Terence Aku, Mark Otieno, Kevin Juma (nahodha), Nahashon Alembi, Benito Kore, Kennedy Ngunjiri na Herman Sikubali. Pia wapo David Aringo, Alex Sunga, Michael Onyango, Washington Vihembo, Kweyu Edward, Kennedy Odhiambo na Frank Abor.

Kangemi Wazoefu ndio iliyokuwa bingwa mtetezi lakini ilibanduliwa kwenye mechi za mchujo. Mashindano ya mwaka 2020 yalijumuisha jumla ya timu 95, 78 na 17 za wanaume na wanawake mtawalia.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Wahudumu wa matatu wapuuzao kanuni za kuzuia corona...

Wahudumu wa matatu washauriwa walipishe nauli ifaayo bila...