• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Udukuzi: Owalo asema data za Wakenya ziko salama

Udukuzi: Owalo asema data za Wakenya ziko salama

NA KASSIM ADINASI

WAZIRI wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, Eliud Owalo, amesema kutakuwa na mikakati na mifumo madhubuti ya kulinda data za Wakenya kuzuia jaribio lolote la udukuzi unaolenga wavuti na majukwaa mengine ya mtandaoni yanayomilikiwa na serikali.

Mapema wiki hii, Wakenya wengi walitatizika kupata huduma muhimu za usajili wa watoto wanaozaliwa na vifo, cheti cha mienendo almaarufu ‘good conduct’, usajili wa biashara, huduma za paspoti na miongoni mwa huduma nyinginezo baada ya jukwaa la e-Citizen kudukuliwa.

Lakini sasa Bw Owalo amesema Jumamosi akiwa katika Shule ya Wasichana ya Ng’iya kwamba jaribio hilo halitasitisha harakati za serikali ya Kenya Kwanza kuhakikisha huduma muhimu zinahamishwa katika majukwaa ya mtandaoni.

Waziri Owalo amesema hayo akizindua maabara ya kidijitali katika shule hiyo ya wasichana.

“Tumeweka mifumo kinga madhubuti kulinda data za Wakenya dhidi ya vitisho vya wadukuzi,” amesema waziri Owalo.

Ameeleza kwamba kile wadukuzi walifanya kwa e-Citizen ni kuleta msongamano wa huduma hiyo wakati wa jaribio la udukuzi. Kundi linalofahamika kama “Anonymous Sudan” lililenga e-Citizen yenye zaidi ya 5,000 zinazotolewa na mashirika ya serikali, wizara mbalimbali, na serikali za kaunti.

Waziri Owalo anatarajiwa kufungua maabara ya kidijitali katika shule ya Lwak Girls iliyoko Rarieda, na Asumbi Girls kufikisha shule tano katika eneo la Nyanza ikizingatiwa kwamba awali alishazindua maabara ya kisasa katika Maseno School na St Marys Yala.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Mlima Kenya: Hongo ya Sh7m kwa siku ulevi utande bila...

Miss Independents watoa Sh300,000 wapachikwe mimba

T L