• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:03 PM
Uhalifu: Kilabu cha burudani Nairobi ambapo simu za walevi hazipumui 

Uhalifu: Kilabu cha burudani Nairobi ambapo simu za walevi hazipumui 

NA SAMMY WAWERU

KILABU cha burudani mtaa wa Zimmerman, Nairobi kinamulikwa kwa kuchangia visa vya uhalifu mmiliki akidaiwa kushirikiana na wahuni. 

Baa hiyo maarufu imesemekana kuwa ngome ya wahalifu hasa wezi wa simu. 

Mmiliki analaumiwa kwa kutoweka mazingira salama hatua ambayo imechangia kukithiri kwa wahuni wanaopora wateja na hata wahudumu. 

“Baadhi yetu tumepoteza simu, mwajiri akikosa kutusaidia kutambua wezi kupitia kamera za siri (CCTV),” Catherine Githinji, mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wake akaambia Taifa Leo Dijitali kupitia mahojiano ya kipekee. 

Mhudumu huyo alilalamikia mmiliki wa Kilabu hicho kuweka CCTV ambazo hazifanyi kazi.

Hilo lilifichuka baada ya Catherine na mfanyakazi mwenza kuporwa simu, na alipotakiwa kutoa video kutambua waliotekekeza wizi huo alikiri CCTV zake hazifanyi kazi. 

“Alilazimika kuzishughulikia baada ya mambo kuchacha,” Catherine akaarifu.  

Katika mojawapo ya visa, simu ya mfanyakazi iliyoibwa ilipofuatiliwa na askari, mawimbi yake yalionekana katika jengo la kibiashara la China Square, Thika Super Highway. 

Kituo hicho cha kibiashara kimepakana na Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU). 

“Tumekuwa tukiifuatilia na mara ya mwisho mawimbi yalionekana China Square, kabla ya simu hiyo kuzimwa. Tulipofanya uchunguzi zaidi, tuligundua mhusika ni mtu mwenye rekodi kadha za uhalifu,” akaarifu kachero wa Kitengo cha Uchunguzi wa Uhalifu na Jinai (DCI) aliyeomba kubana majina yake. 

“Tunaendelea kusaka maficho yake,” akasema. 

Aidha, duru zinaarifu wateja wanapozima mwasho wa koo na kulemewa na makali ya pombe jeshi la wezi huanza kupora watu simu. 

Kilabu hicho kipo kati ya Githurai 44 na jumba maarufu la kibiashara la Thika Road Mall (TRM). 

Baada visa vya wizi wa simu kuripotiwa, usimamizi unadaiwa kudhulumu baadhi ya wafanyakazi walipolalamikia kuhusu usalama wao na wa wateja. 

Mmoja wao aliuguza majeraha, tukio hilo likiripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Kasarani. 

Kufikia sasa, hakuna yeyote aliyeshtakiwa kuhusu tukio hilo.

Si mara ya kwanza kilabu hicho kumulikwa na kukwaruzana na mkono wa sheria.

  • Tags

You can share this post!

Embarambamba: Makabila yote Kenya yananipenda, Kisii pekee...

Majengo ya mamilioni ya pesa Eldoret kubomolewa kuigeuza...

T L