• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 5:50 AM
UJAUZITO NA UZAZI: Athari za mimba kuharibika

UJAUZITO NA UZAZI: Athari za mimba kuharibika

NA PAULINE ONGAJI

TATIZO la mimba kuharibika huenda likawakumba asilimia kubwa ya wanawake wakati mmoja maishani, kutokana na sababu moja au nyingine.

Lakini kwa wanawake wengi wanaokabiliwa na shida hii, suluhu huwa kujaribu kusahau na kuendelea na maisha haraka iwezekanavyo.

Wengi hufanya hivyo hata bila kufikiria kuchukua hatua za kiafya ili kutambua kiini chake haswa.

Wataalamu wanasema kwamba ukipoteza mimba huenda kila kitu kikaondoka katika kipindi cha muda mfupi ambapo mwili wako utaanza kupona bila matatizo yoyote.

Hata hivyo, kuna wakati mwingine ambapo mimba hutoka na huenda kitakachosalia tumboni kikasababisha matatizo baadaye kama vile maambukizi, kuvuja damu, au hata tatizo la chupa ya mtoto kushindwa kushikilia mimba kwa miezi tisa.

Kuna wakati kinachosalia huendelea kukua sawa na mimba ya kawaida.

Unapokumbwa na shida hii, litakuwa jambo la busara kwenda hospitalini ili ufanyiwe skeni ya ultrasound kuona iwapo kila kitu kimerejelea hali ya kawaida, au ikiwa kuna kitu kilichosalia ndani ambacho huenda kikakusababishia matatizo baadaye.

Hasa katika masuala ya ujauzito, wataalamu wa uzazi wanasisitiza kwamba ni heri kuwa salama badala ya kujuta.

  • Tags

You can share this post!

Kingi hafai kumlaumu Raila, asema Mung’aro

Eddie Nketiah atia saini mkataba mpya wa miaka mitano...

T L