• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
Umaskini chanzo cha mimba za mapema – Shirika

Umaskini chanzo cha mimba za mapema – Shirika

NA KASSIM ADINASI

UMASKINI na ukosefu wa mahitaji ya kimsingi vinachangia ongezeko la mimba za wasichana walio na umri mdogo na maambukizi ya Ukimwi, Kaunti ya Siaya, inasema ripoti ya shirika lisilo la serikali la Globcom.

Kulingana na mkurugenzi wa shirika hilo Bw Ibrahim Otieno, umaskini unawasukuma wasichana hao kushiriki ngono na wanaume wa umri mkubwa ili wapate mahitaji ya muhimu.

Matumizi ya mihadarati na dhuluma za jinsia pia zinatajwa kuchangia ongezeko la mimba za mapema miongoni mwa wasichana katika kaunti hiyo.

You can share this post!

Tiketi yake Raila na Karua yabisha hodi

Kaunti yafunza wauguzi wake kutambua kansa

T L