• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 5:50 AM
Vihiga Boys ni wafalme wa raga ya Prescott Cup

Vihiga Boys ni wafalme wa raga ya Prescott Cup

NA GEOFFREY ANENE

SHULE ya Upili ya Wavulana ya Vihiga ilijiongezea taji la Kombe la Prescott kwenye kabati lake baada ya kupepeta Kisii High 29-8 katika fainali ugani RFUEA mjini Nairobi, Jumapili.

Vihiga, ambayo inafahamika kutoa wanaraga matata Collins Injera, Oscar Ayodi, Edgar Abere, Shaban Ahmed na Collins Shikoli, iliongoza Kisii 7-5 wakati wa mapumziko kabla ya kuzidia wapinzani wao ujanja kabisa katika kipindi cha pili.

Timu hizo zilikuwa zimeshinda makundi yao bila kupoteza.

Kisii walimaliza juu ya Kundi A baada ya kukung’uta Ofafa Jericho 13-12, Maseno 8-6 na Utumishi 6-0.

Waliingia nusu-fainali kutoka kundi hilo pamoja na Ofafa Jericho. Vihiga walitawala Kundi B walipochbanga Jomo Kenyatta 22-7, Mang’u 26-3 na Kangaru 34-0.

Walijikatia tiketi ya nusu-fainali pamoja na Jomo Kenyatta. Kisii ilitinga fainali baada ya kulipua Jomo Kenyatta 18-0 nao Vihiga, ambao Agosti walinyakua taji la raga ya wachezaji saba kila upande ya shule za upili, walizima Ofafa 24-5.

Mabingwa wa makala yaliyopita Upper Hill hawakushiriki mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika majuma machache baada ya wasichana ambayo St Mary’s Mabera kutoka Migori ilinyamazisha Eregi kutoka Kakamega 14-10 katika fainali mjini Nakuru.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Njaa: Ruto, Raila wasaidie nchi kutafuta...

Faida za kiafya za kuruka kamba

T L