• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 2:25 PM
VINYWAJI: Faida za juisi mbalimbali

VINYWAJI: Faida za juisi mbalimbali

Na MARGARET MAINA

[email protected]

JUISI ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha kama ya matunda lakini si matunda.

Vinywaji hivyo igizi mara nyingi huongezwa sukari na kemikali nyingine za kuhifadhia (preservertives) ili zisiharibike; kitu ambacho kiafya hakikubaliki.

Juisi ya karoti, kitunguu saumu na tufaha

Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu saumu na tufaha husafisha mwili na huondoa sumu mwilini na kuupa mwili nguvu.

Tango na figili

Juisi ya mchanganyiko wa tango na mboga ya majani aina ya Figili (celery) hupunguza lehemu mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kichwa kuwanga.

Nyanya na karoti

Juisi ya mchanganyiko wa nyanya na karoti huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.

Chungwa, tangawizi na matango

Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.

Nanasi na tikitimaji

Juisi ya mchangayiko wa nanasi na tikitimaji huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba juisi hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.

Papai, nanasi na maziwa

Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni.

Juisi aina hizi humpa mnywaji kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

You can share this post!

Ighalo ashangazwa na mazoezi chini ya masharti mapya

Leicester City kukimbilia Bertrand

adminleo