• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Vipusa 3 wakamatwa Murang’a wakinengulia walevi viuno wakiwa uchi kwenye baa  

Vipusa 3 wakamatwa Murang’a wakinengulia walevi viuno wakiwa uchi kwenye baa  

NA MWANGI MUIRURI 

MAAFISA wa polisi katika Kaunti ya Murang’a wamevamia baa moja na kunasa wanawake watatu waliokuwa wakinengulia walevi viuno, wakiwa uchi wa mnyama.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Murang’a Mashariki, Bi Mary Kasyoki, watatu hao walinaswa mnamo Ijumaa, Septemba 1, 2023 mwendo wa saa saba usiku wakiridhisha macho ya walevi wa kiume kwa kuwasakatia densi wakiwa uchi.

“Watatu hao walinaswa katika baa ya mwanamke ambaye anafahamika kama Wambui wa Maguna, ikifahamika kama Orpul. Tulipata dokezi kwamba kulikuwa na mambo ya kustaajabisha na tilipotuma maafisa kujua hali, wakakumbana na uchi wa watatu hao,” akasema.

Bi Kasyoki alisema maafisa wa kiume walijitoa na wakapisha wenzao wa kike washughulikie kisa hicho.

Alisema washukiwa walionaswa, watafunguliwa mashtaka mnamo Jumatatu, Septemba 4 kwa ukiukaji wa maadili katika jamii kwa kuvua nguo eneo la umma.

Hata hivyo, mabishano kati ya polisi na walevi wa kiume yalizuka ambapo wateja walilia kwamba hawakuwa wakilalamika kuonyeshwa uchi.

“Sisi tumelipa ili tuone hayo mnayoharamisha. Mmekuja sehemu ambayo hamfai kuwa. Huku sisi starehe yetu ni hii na hamfai kutupimia hewa ya burudani,” akafoka mmoja wa walevi.

Lakini kamanda wa polisi wa Kituo cha polisi cha Murang’a, Bw Patrick Lumumba alisikika akisema kwamba “hili ni taifa la uaminifu kwa sheria na hakuna aliye na ruhusa kuanikia umma uchi wake kwa sababu yoyote ile”.

Bw Lumumba alisema kwamba maadili ya kijamii ni lazima yadumishwe, akionya kuwa huenda leseni ya baa hiyo ipendekezwe kutwaliwa na serikali.

Wenyeji wamekuwa wakiteta mara kwa mara kuhusu kelele ambazo baa hiyo hupiga usiku kucha, na pia wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kujumuika kama wateja.

Kelele za baa hiyo zimetajwa kuunda jukwaa la uporaji wa simu na pesa.

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Mahindi: Wakulima Bonde la Ufa katika njiapanda

Karen Nyamu: Samidoh alinichagua kwa sababu huvalia...

T L