• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 6:55 PM
Wachezaji 10 wa EPL katika orodha ya chipukizi 100 wanaowania tuzo ya Golden Boy mwaka huu

Wachezaji 10 wa EPL katika orodha ya chipukizi 100 wanaowania tuzo ya Golden Boy mwaka huu

Na MASHIRIKA

WACHEZAJI 10 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na Waingereza wengine watatu wako katika orodha ya chipukizi 100 wa kwanza wanaowania taji la Golden Boy mwaka huu.

Mnamo 2020-21, Pedri wa Barcelona ndiye alishinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa mchezaji aliye na umri wa chini ya miaka 21 miongoni mwa Ligi Kuu za bara Ulaya.

Manchester United, Liverpool na Wolves wana wachezaji wawili kila mmoja kwenye orodha hiyo itakayokuwa ikipunguzwa kila mwezi.

Mshindi wa tuzo hiyo ataamuliwa kwa kura zitakazopigwa na wanahabari barani Ulaya na mashabiki kwenye tovuti ya waandalizi, Tuttosport.

Mbali na Eduardo Camavinga wa Real Madrid, wanasoka wengine wanaopigiwa upatu wa kutwaa taji la Golden Boy mwaka huu ni Gavi wa Barcelona, Jamal Musiala wa Bayern Munich na Jude Bellingham wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uingereza.

Wawaniaji wa tuzo hiyo kutoka EPL ni: Amad Diallo, Anthony Elanga (wote wa Man-Utd), Harvey Elliott, Fabio Carvalho (wote wa Liverpool), Fabio Silva, Ki-Jana Hoever (wote wa Wolves), Yan Couto (Man-City), Joe Gelhardt (Leeds), Kacper Kozlowski (Brighton) na Pape Matar Sarr (Tottenham).

Beki wa kulia wa Brazil, Couto, kiungo Kacper Kozlowski wa Poland, fowadi wa Senegal, Sarr na Carvalho ambaye ni sajili mpya wa Fulham wako katika orodha hiyo licha ya kutochezea waajiri wao wa EPL kufikia sasa.

Bellingham, Elliott, Gelhardt na Noni Madueke wa PSV Eindhoven ni miongoni mwa wachezaji wa Uingereza katika orodha hiyo ya 100-bora. Aaron Hickey wa Bologna ndiye mchezaji wa pekee kutoka Scotland kwenye orodha hiyo.

Baadhi ya washindi wa zamani wa tuzo hiyo walioshia kuwa masogora maarufu ni Wayne Rooney, Lionel Messi, Raheem Sterling, Kylian Mbappe na Erling Haaland.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Misri wamtimua kocha Ehab Galal baada ya kusimamia mechi...

Difenda Dani Alves kuagana na Barcelona kwa mara ya pili

T L