• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 5:55 AM
Wanajeshi 1, 000 wa Burundi walitumwa kisiri mashariki mwa DRC

Wanajeshi 1, 000 wa Burundi walitumwa kisiri mashariki mwa DRC

NA MASHIRIKA

ZAIDI ya wanajeshi 1, 000 wa Burundi walitumwa kisiri Mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Oktoba, 2023.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) isiyochapishwa, wanajeshi hao wamekuwa wakivalia magwanda ya wanajeshi wa DRC wakishirikiana nao kupambana na waasi wa M23.

Huku ikinukuu duru za usalama na ujasusi na maafisa walio karibu na kamanda wa jeshi la DRC, ripoti hiyo iliyotayarishwa na Wataalamu wa UN nchini humo inasema wanajeshi hao walisafirishwa kutoka Burundi hadi Mashariki mwa nchi hiyo na ndege za jeshi la DRC.

Walisafirishwa kuanzia Septemba 21 hadi Oktoba 12.

Serikali za Burundi na DRC hazikutoa kauli zozote kuhusu ufichuzi huo.

 

Tafsiri Na Charles Wasonga 

 

  • Tags

You can share this post!

Wafuasi wa UDA, Jubilee walimana mangumi Nyahururu

Daddy Owen afunguka kuhusu uhusiano wake na Charlene Ruto

T L