• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 5:20 PM
WANDERI KAMAU: Adhabu kali dhidi ya msanii Kelly onyo kwa wachafuao watoto

WANDERI KAMAU: Adhabu kali dhidi ya msanii Kelly onyo kwa wachafuao watoto

NA WANDERI KAMAU

KUFUNGWA gerezani kwa mwanamuziki maarufu Robert Kelly nchini Amerika, kumedhihirisha kwamba hatimaye dunia imeanza kuzinduka kuhusu haki za watoto.

Kelly alihukumiwa miaka 30 gerezani kwa kupatikana na hatia ya kuwadhulumu kingono watoto wa umri chini ya miaka 18.

Hukumu yake inajiri baada ya baadhi ya watu maarufu nchini humo pia kukabiliwa na visa kama hivyo.

Baadhi yao ni marehemu Michael Jackson, aliyekuwa miongoni mwa wanamuziki maarufu zaidi katika karne ya 20.

Wakati wa kifo chake mnamo 2009, kesi yake ilikuwa bado inaendelea mahakamani kuhusiana na tuhuma hizo.

Kwa miaka mingi, mataifa ya Magharibi yamekuwa yakilaumiwa kwa kutochukua hatua za kutosha kuwaadhibu watu wanaopatikana na hatia za kujihusisha kwenye vitendo vya dhuluma za kimapenzi—iwe ni dhidi ya watoto, wanawake ama wanaume.

Ni taswira ambayo imeharibia sifa mataifa hayo kama jukwaa la ukiukaji wa haki za binadamu.

Hata hivyo, hukumu kali dhidi ya mwanamuziki Kelly inadhihirisha kuwa hatimaye nchi hizo zimeanza kujinasua kutoka kwa dhana hizo za jadi.

Ni hukumu ambayo pia inapaswa kuzifungua macho nchi za Afrika na kwingineko duniani, kwamba hazipaswi kamwe kusaza watu wanaokabiliwa na tuhuma kama hizo.

Nchini Kenya, kumekuwa na visa vya kila aina vya watu maarufu wanaoshirikiana na maafisa wa mahakama ili kuwalinda dhidi ya kuadhibiwa kwa kupatikana na makosa kama hayo.

Wito mkuu ni kwa Idara ya Mahakama nchini kujifunza na mfumo wa utoaji haki nchini Amerika, kuhusu njia ya kuwaadhibu wale wanaopatikana na hatia za kushiriki kwenye vitendo kama hivyo.

  • Tags

You can share this post!

Ruto, Raila sasa waibiana ahadi

DOUGLAS MUTUA: Siri ya kuandaa uchaguzi huru ni kuheshimu...

T L