• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Wanyamapori wetu ni zawadi kutoka kwa Mola, tuilinde – Mama wa Taifa

Wanyamapori wetu ni zawadi kutoka kwa Mola, tuilinde – Mama wa Taifa

PSCU na CHARLES WASONGA

MAMA wa Taifa Margaret Kenyatta amekariri umuhimu wa Wakenya kuhakikisha wanalinda wanyama pori kwa manufaa ya kiuchumi na vizazi vijavyo, akisema hao ni rasilimali ya kipekee inayotambulisha Kenya kati ya mataifa ya ulimwengu.

Alisema aina mbalimbali za wanyama pori wanaopatikana humu nchini, kama vile ndovu na faru, ni zawadi maalum kwa taifa hili kutoka kwa Mungu.

Kwa hivyo Mkewe Rais alisema alisema Wakenya watakuwa wakihujumu uchumi wa nchini na masilahi ya vizazi vijavyo ikiwa hawatalinda ndovu na faru dhidi ya wahalifu ambao wanalenga kuwaangamiza.

“Tukifeli kulinda wanyama hawa, haswa ndovu na vifaru ili wasiangamizwe kabisa, walivyotabiri wanamazingira, basi tutakuwa tumekosea vizazi vijavyo- watoto wetu na watoto wa watoto wetu,” akasema Bi Kenyatta.

Mama wa Taifa alisema hayo Jumamosi mjini Nanyuki wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 35 tangu kuanzishwa kwa wakfu wa kulinda wanyamapori kwa jina, William Holden Wildlife Foundation (WHWF).

Mwasisi wa wakfu hiyo Marehemu William Holden, ambaye pia alikuwa mwigizaji mashuhuri wa filamu nchini Amerika, aliwahi kupata tuzo kadhaa kutoka na juhudi zake za kulinda wanyamapori.

Alizuru Kenya mnamo 1954, akavutiwa na wanyamapori nchini, ndipo akaamua kutumia wakati wake kuendeleza utunzaji wa wanyama hao kupitia Mbuga ya Wanyamapori ya Mlima Kenya.

You can share this post!

Kenya yaumizwa 2-0 na Morocco soka ya UNAF Misri

Joho ametosha mboga kuongoza Kenya 2022, asema Atwoli

adminleo