• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
Washukiwa 10 wakamatwa kwa kuiba mali ya Sh3 milioni kutoka kwa bohari

Washukiwa 10 wakamatwa kwa kuiba mali ya Sh3 milioni kutoka kwa bohari

Na SAMMY KIMATU

WASHUKIWA 10 walikamatwa katika wikendi ya shamrashamra za Krismasi walipopatikana wakiiba mali ya thamani ya Sh3 milioni katika Eneo la Viwanda jijini Nairobi.

Mkuu wa polisi Eneo la Makadara, Bw Timon Odingo alisema washukiwa wote walikuwa ni wanaume ambao walipangiwa njama ya wizi huo na mlinzi katika eneo la kisa.

“Kulikuwa na mlinzi aliyekuwa amefutwa kazi kwa jina Bw Oscar Wanjala, 28 akishirikiana na mlinzi mwingine kwa jina Bw Alfred Ratemo waliopanga wizi wa vifaa katika bohari lililoko mkabala wa barabara ya Road C,” Bw Odingo akasema.

Miongoni mwa vifaa vilivyopatikana ndani ya gari aina ya Mitsubishi Canter KAP 805 W ni pamoja na mashine ya kudhibiti joto yaani air conditioner na vifaa vya kuchunga mafuta ya injini za magari yaani oil filters.

Bw Odingo alisema washukiwa walifumaniwa na polisi mwendo wa saa mbili usiku baada ya msimamizi wa kampuni ya ulinzi alipoona kitu kikirushwa kutoka nje ya kampuni na kuanguka upande wa ndani.

“Msimamizi huyo aliwapigia simu maafisa wangu na mara moja wakakimbia na kuzingira eneo la kisa,” Bw Odingo akaambia Taifa Leo.

Isitoshe, Bw Odingo aliongeza kwamba gari lililotumiwa kupakiwa vifaa vilivyoibwa lilinaswa na kukokotwa hadi katika kituo cha polisi cha Industrial Area.

Washukiwa nao walifungiwa ndani ya seli wakisubiri kufikishwa kortini mnamo Jumanne wiki ijayo.

  • Tags

You can share this post!

Mbappe na Lewandowski wapinga mpango wa FIFA kuandaa Kombe...

Jinsi wakazi wa Nairobi walivyosherehekea Krismasi bila...

T L