• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 12:48 PM
William Kabogo akumbuka kanisa la alikozaliwa

William Kabogo akumbuka kanisa la alikozaliwa

NA SAMMY WAWERU

ALIYEKUWA Gavana wa Kiambu, William Kabogo mnamo Jumapili, Agosti 13, 2023 aliungana na waumini wa Kanisa la PCEA, Gituamba, Githunguri ambapo alishiriki mchango kukuza nyumba ya Mungu.

Kupitia chapisho la Facebook, Bw Kabogo alipakia picha kadha za ushirika huo akidokeza kwamba ni kanisa la nyumbani anakotoka.

“Nilijiunga katika hafla ya kuchangisha pesa Kanisa la P.C.E.A Gituamba, Parokia ya Karuthi, eneobunge la Githunguri kusaidia kuliboresha. Ni kanisa la eneo ninalotoka (akiashiria alikozaliwa),” akaandika kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook.

Chapisho la Gavana huyo wa kwanza Kiambu, pia liliandamana na fungu la Biblia, Kitabu cha Wakorintho Nakala ya 2, kifungu cha 9 Mstari wa 7.

“Kila mtu lazima atoe kama walivyochagua mioyoni mwao, si kwa kukataa au kwa kulazimishwa, maana Mungu humpenda mtoaji mchangamfu. Pamoja, tunajenga nyumba yake ya ibada, tukidumisha imani yetu na jamii.”

Aliyekuwa Gavana wa Kiambu, Bw William Kabogo akitoa mchango wake kusaidia kuboresha Kanisa la P.C.E.A Gituamba, Parokia ya Karuthi, eneobunge la Githunguri. PICHA|HISANI

Katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022 Bw Kaboko aliwania kiti cha ugavana Kiambu kupitia chama chake cha Tujibebe Wakenya.

Mwanasiasa huyo, hata hivyo, hakufua dafu.

Aliibuka wa tatu kwa kura 106, 980 katika kinyang’anyiro ambacho Bw Kimani Wamatangi wa United Democratic Alliance (UDA) alitwaa ugavana Kiambu kwa kuzoa kura 348, 371.

Wengine walikuwa Bw James Nyoro, gavana wa tatu Kiambu aliyepata 99, 562 kupitia tikiti ya chama cha Jubilee, Patrick Wainaina Wa Jungle akiwa wa pili na kura 237,361.

Tangu abwagwe, Bw Kabogo hajakuwa akijitokeza sana hadharani na maeneo ya umma.

  • Tags

You can share this post!

Ndoa na familia za walimu sasa kuimarika

Wamaua asikitishwa na tabia za wanaume kubaka watoto

T L