• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Yatani aahidi kutekeleza Ajenda Nne Kuu

Yatani aahidi kutekeleza Ajenda Nne Kuu

Na CHARLES WASONGA

KAIMU waziri wa Fedha Ukur Yatani amemshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kumteua kwa wadhifa huo, huku akitoa ahadi ambazo atatekeza katika wadhifa huo.

Akiongea na wanahabari Jumatano saa chache baada ya kuteuliwa kwa wadhifa huo aliahidi kushirikiana na wenzake kutekeleza ajenda nne kuu za serikali.

“Nitamsaidia Rais katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuendesha nchini kwa kutekeleza kikamilifu majukumu yote ya afisi ya Waziri wa Fedha,” akasema Bw Yatani.

Akaongezea: “Nafahamu kuwa kibarua kilichoko mbele yangu ni kubwa. Na matarajio ya Wakenya kwangu pia ni mengi. Lakini nitahakikisha kuwa uchumi uko sawa kwa kuupa kipaumbele utekelezaji wa Ajenda Nne Kuu za Serikali.”

Waziri Yatani pia alisema atahakikisha kuwa nidhamu inadumishwa na wafanyakazi wot echini yake katika wizara ya Fedha.

“Uteuzi wangu unajiri wakari ambapo kuna masuala mengi ya uongozi kushughulikiwa sio tu katika Wizara ya Fedha bali katika serikali yote. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa nimezishughulikia ipasavyo,” akasema.

Uteuzi wa Bw Yatani ulitangazwa kupitia taarifa iliyotumwa kwa vyumba vya habari na msemaji wa Ikulu Bi Kanze Dena.

“Ili kuhakikisha kuendelea kwa shughuli za Serikali bila shida yeyote na kutimizwa kwa majukumu katika Hazina ya Kitaifa na Wizara husika kufuatia agizo la Mahakama linalomhusu Waziri wa Hazina ya Kitaifa na Mipango Bw Henry Rotich na Katibu wa Hazina ya Kitaifa Dkt Kamau Thugge, Rais amefanya mabadiliko yafuatayo Serikalini:

Mheshimiwa Balozi, Ukur Yatani Kanacho, ambaye ni Waziri wa Masuala ya Wafanyakazi na ya Kijamii, pia atakuwa kaimu Waziri wa Hazina ya Kitaifa na Mipango

Dkt. Julius Monzi Muia ameteuliwa kuwa Katibu katika Wizara ya Hazina ya Kitaifa.

Bw. Torome Saitoti ameteuliwa kuwa Katibu katika Idara ya Mipango.

Meja Mstaafu Jenerali Gordon Kihalangwa ameteuliwa kuwa Katibu katika Wizara ya Ulinzi.” akasema Dena.

You can share this post!

Mradi wa mikoko Kwale wasaidia katika uhifadhi wa mazingira

Sonko ampa kazi dadake Raila

adminleo