Habari za Kitaifa

Vituo vya petroli vinavyoogelea maji ya mafuriko vifungwe – Epra

May 2nd, 2024 1 min read

NA JOHN MUTUA

SERIKALI imeagiza wamiliki wa vituo vya petroli vilivyo katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wavifunge ili kudhibiti uuzaji wa mafuta yaliyochanganyika na maji.

Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli (Epra) ilitangaza uamuzi huo Jumatano ikiwa ni hatua ya kuwalinda madereva dhidi ya kununua mafuta yaliyochanganyika na maji ambayo huharibu injini za magari.

Mbali na kuharibu miundombinu, kuleta maafa na kujeruhi wengi, mafuriko hayo pia yameziba tangi iliyochimbwa chini kuhifadhi Mafuta (UST).

“Vituo vinavyouza petroli vilivyo katika maeneo ambayo yameathiriwa na mafuriko vinafaa kufungwa. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa madereva au wateja wanapata mafuta bora,” Mkurugenzi Mkuu wa Epra Daniel Kiptoo alisema kwenye notisi.