Washirika

Nathan Digital yapanua shughuli zake; yaanzisha kitengo kipya Nairobi

Na MWANDISHI WETU January 14th, 2025 Kusoma ni dakika: 2

NATHAN Digital, ambayo ni tawi la kiteknolojia la kampuni ya Nathan Investments Holdings iliyo na makao makuu Dubai, inajivunia kutangaza mkondo mwingine wa ukuaji wake wa kimataifa kwa uzinduzi wa kituo chake cha uundaji wa programu za kompyuta jijini Nairobi, Kenya.

Hatua hii muhimu inatoa fursa katika ukuaji wa kampuni katika mauzo ya programu nchini Kenya na katika mataifa mengine Afrika, utakaoanza katika robo ya kwanza ya mwaka wa 2025.

Mandhari ya ndani ya Nathan Digital Nairobi Hub, kitengo kipya kabisa cha uundaji na uvumbuzi wa programu za kompyuta. Picha|Hisani

Nathan Investment Holdings ni kampuni iliyo na operesheni nyingi na ina uwepo katika idara nyingi kama vile uundaji programu na teknolojia, uhandisi, shughuli rasmi za kikazi, usimamizi wa wafanyakazi, ukandarasi wa kujisimamia, uchapishaji wa 3D, viwanda, biashara na usambazaji, pamoja na viwanda vya kilimo.

Huku kukiwa na zaidi ya wafanyakazi 200 na kuanzishwa kwa kituo kikubwa cha kuunda programu, mpango wa mauzo utaanza robo ya kwanza ya mwaka 2025

Kituo cha Nairobi Hub ambacho kilizinduliwa mwishoni mwa 2023, ni uwekezaji mkubwa katika muundomsingi wa hali ya juu na talanta nchini Kenya. Kufikia sasa, Nathan Digital imeajiri zaidi ya wafanyakazi 200 walio na ujuzi wa hali ya juu na kuna mpango wa kuongeza wafike 500 kufikia mwisho wa 2025.

Kujitolea kwetu kukuza talanta na uvumbuzi

Wafanyakazi wa Nathan Digital katika kitengo cha Nairobi Hub wakimakinika kazini. Picha|Hisani

“Tuna furaha kupanua uwepo wetu Kenya kwa kuendeleza ufanisi tuliopata katika kituo chetu cha uundaji programu cha Nairobi,” asema Rohan Nathan, Afisa Mkuu Mtendaji wa Nathan Digital.

“Huku tukiwa na afisi ya ukubwa futi mraba 32,000 eneo la Westlands, kituo hiki ndio nguzo ya operesheni zetu. Kujitolewa kwa kikosi chetu kumeweka msingi thabiti wa ukuaji, na tunapanga kuongeza nguvukazi hadi 500 kufikia katikati ya mwaka ili kupiga jeki mipango yetu kimataifa.”

Kitengo cha Nairobi kinadhihirisha kujitolea kwa kampuni ya Nathan Digital kukuza uvumbuzi wa kiteknolojia, kuendeleza mabadiliko, kukuza vipaji nchini Kenya na Afrika kwa jumla.

Uwepo wetu kimataifa unavyoifaa jamii nyanjani

Jengo la The Piano, ambalo afisi za Nathan Digital Nairobi Hub ziko, eneo la Westlands. Picha|Hisani

Upanuzi wa Nathan Digital sio wa Afrika pekee. Kampuni pia ina uwepo Uingereza, Amerika, Canada, Ireland, Singapore na Afrika Kusini. Mauzo ya programu yatafanyika mwaka wote wa 2025, na kutoa fursa ya ukuaji zaidi na nafasi za ajira.

Ufanisi katika masoko haya unatarajiwa kuongezea nguvu mipango ya upanuzi na kuwapa wafanyakazi wa Nathan Digital manufaa zaidi.

Kuangalia Mbele

Ikiwa sehemu ya misheni yake ya kuongoza katika ulingo wa teknolojia, Nathan Digital inaendelea kuwekeza kwenye maeneo ambako inahudumu. Kwa kutumia Kitengo kipya cha Nairobi, kampuni iko kwenye nafasi nzuri ya kuendeleza utoaji wa suluhu za uvumbuzi wa kiteknolojia na kuleta manufaa ya kudumu ya kiuchumi.

Kwa habari zaidi kuhusu huduma za Nathan Digital, tafadhali wasiliana na Grace Kimbe, katika [email protected] au tembelea www.nathandigital.com.