• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:27 PM
Kocha wa Nigeria aanikwa kupokea hongo

Kocha wa Nigeria aanikwa kupokea hongo

Na Geoffrey Anene

KOCHA wa Super Eagles ya Nigeria, Salisu Yusuf, amemwaga unga kwa kupokea fedha kutoka kwa mwanahabari kutoka Ghana, Anas Aremeyaw Anas, ambaye alianika refa Mkenya Aden Range Marwa kabla tu ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Kufuatia ufichuzi dhidi ya Yusuf, Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limepiga Yusuf, ambaye ni naibu wa Mjerumani Gernot Rohr, marufuku miezi 12 na faini ya Sh503,750 kwa kupokea fedha kutoka kwa mwanahabari huyo aliyejifanya ni wakala.

Taarifa nchini Nigeria zinasema kwamba Kamati ya Maadili ya NFF imepata Yusuf na hatia ya kupokea Sh100,740 baada ya kunaswa kwenye video akiombwa kujumuisha wachezaji wawili katika kikosi cha Soka ya Afrika ya wachezaji wanaosakata katika mataifa yao (CHAN) mwaka 2018.

“Tumempiga marufuku mwaka mmoja na faini ya Sh503,750, ambayo lazima alipe chini ya miezi mitatu kutoka tarehe ya uamuzi huu,” NFF imesema.

Yusuf, ambaye amekanusha madai ya kufanya kosa, ana fursa ya kukata rufaa.

Anas alianika refa bora wa Kenya mwaka 2017, Marwa, ambaye mwalimu wa somo la hisabati na kemia katika Kaunti ya Migori, akipokea hongo ya Sh60,000 kupanga matokeo ya mechi moja ya CHAN nchini Morocco.

Marwa anatumia marufuku ya maisha ya kutojihusisha na soka. Ufichuzi mwingine wa mwanahabari huyo pia ulipelekea kujiuzulu kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Ghana, Kwesi Nyantakyi, aliyedaiwa kuitisha hongo.

You can share this post!

Maiti ya mwanachuo mjamzito yapatikana msituni

Mahakama yasitisha ushuru wa 16% kwa muda

adminleo