• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:27 PM
Wito kwa wasomi waungane kutatua kiini cha maziwa kufurika

Wito kwa wasomi waungane kutatua kiini cha maziwa kufurika

Na MAGDALENE WANJA

WANASAYANSI nchini bado hawajapata sababu halisi ya kufurika kwa maziwa ya Bonde la Ufa.
Maziwa hayo haswa lile la Nakuru yanaendelea kushuhudia ongezeko la maji kila siku huku madhara yake yakiendelea kuonekana.
Akizungumza alipozuru Mbuga ya Wanyama ya Nakuru, Gavana Lee Kinyanjui aliwataka wanasayansi haswa kwenye vyuo vikuu kuungana na wenzao katika kutafuta suluhisho la kufurika kwa maziwa hayo ambako kumeshuhudiwa kwa miaka mitano sasa.
“Tungetaka ushirikiano na watafiti kwenye vyuo vikuu katika kutafuta majibu kuhusu kufurika kwa maziwa ya Bonde la Ufa,” alisema Bw Kinyanjui.
Baadhi ya wanasayansi wamehusisha kufurika kwa maziwa hayo na kuzorota kwa mazingira kunakotokana na shughuli za kila siku za binadamu.
Baadhi yao poa wamehusisha kufurika huko na shughuli za uchimbaji wa mawe ya nishati ya mvuke ambao ulianza mnamo mwaka 2012.  Ni katika miaka ya 2012-2013 ambapo visa vya kufurika kwa maziwa kulianza kushuhudiwa.
Baadhi ya maziwa mengine ambayo yamefurika ni Baringo, Bogoria na Elementaita.

You can share this post!

Magunia 11 ya bangi yanaswa, mlanguzi ahepa

Afisa wa Engen kizimbani kwa kuiba mafuta ya Oilibya

adminleo