• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 1:14 PM
Afisa wa Engen kizimbani kwa kuiba mafuta ya Oilibya

Afisa wa Engen kizimbani kwa kuiba mafuta ya Oilibya

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA mkuu wa utendakazi katika kampuni ya kuuza mafuta  ya Engen alishtakiwa Jumatatu kwa kuiba bidhaa za mafuta ya petroli ya kampuni ya Oilibya yenye thamani ya Sh237 milioni.

Bw Jadiel Muchui Githinji alikanusha shtaka la kuibia kampuni ya Oillibya mafuta ya petroli na bidhaa nyinginezo zenye thamani ya Sh237,585,492 kati ya Januari 2013 na Septemba 2014.

Bw Githinji aliomba aachiliwe kwa dhamana. Kiongozi wa mashtaka Bi Kajuju Kirimi hakupinga ombi hilo.

Aliomba korti izingatie kiwango cha mafuta ambacho mshtakiwa anadaiwa ameiba ikimwachilia.

Hakimu mkuu Bw Francis Andayi alimwamuru mshtakiwa alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh1 milioni.

Kesi iliorodheshwa kusikizwa mnamo Oktoba 3.

You can share this post!

Wito kwa wasomi waungane kutatua kiini cha maziwa kufurika

Kupanga uzazi kunaipunguzia TZ watu, Magufuli aonya wanawake

adminleo