• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:10 PM
Mtaala mpya waidhinishwa na waangalizi wa kimataifa

Mtaala mpya waidhinishwa na waangalizi wa kimataifa

Na CECIL ODONGO

WAANGALIZI wa Kimataifa wameidhinisha mtaala mpya wa elimu unaoendelea kufanyiwa majaribio katika shule mbalimbali nchini, hii ni kulingana na ripoti ya kamati iliyoundwa na wizara ya elimu kutathmini ufaafu wa mtaa huo iliyowasilishwa jana kwa Waziri wa elimu Amina Mohamed.

“Kiwango cha utekelezaji wa mtaala huo ni asilimia 56, sita juu ya kiwango kilichowekwa ulimwenguni cha asilimia 50. Hii ina maana kwamba thamani yetu ya utekelezaji wa mtaala huo ni ya kupigiwa mfano,” akasema Waziri wa elimu Bi Amina Mohamed

Akizungumza katika mkutano ambao pia uliwashirikisha washikadau wa sekta ya elimu katika Taasisi ya Ukuzaji Mitaala nchini(KICD) jijini Naairobi, Bi Mohamed alisema kwamba shule ambazo zinatumika kwa majaribio ya mtaala huo vile vile zimeripoti ufanisi wa asilimia 64 kulingana na ripoti hiyo.

Aidha Bi Mohamed aliondoa hofu ya kutokuwepo kwa vitabu vya kufundishia mtaala huo kwa wanafunzi wanaofuzu kutoka darasa la tatu hadi nne (Grade 3 hadi Grade 4) akisema mikakati inaendelea kuwekwa ili vitabu hivyo viwe tayari kabla ya mwezi Januari kuzuia kusambaratika kwa mfumo huo mpya wa elimu.

“Hakuna haja ya kuhofia kuhusu tatizo la vitabu kwa sababu wizara iko mbioni kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaoingia grade 4 wanapata vitabu hivyo kufikia mwezi Januari mwaka ujao,” akasisitiza Bi Mohamed.

Vile vile waziri huyo aliongeza kwamba walimu wa madarasa ya chini kote nchini wamepokezwa mafunzo maridhawa kuwawezesha kuwanaoa wanafunzi kwa kuwa mfumo mpya wa 2-6-3-3-3 unazingatia sana maendeleo ya mwanafunzi badala ya 8-4-4 aliyosema imeibua ushindani kwa kujikita sana kupasi mitihani ya kitaifa.

Akigusia matayarisho ya KCPE na KCSE zinazotarajiwa kuanza baadaye mwezi huu na mwezi ujao mtawalia, Bi Mohamed alifichua kwamba shule zaidi zinaendelea kuchunguzwa kuhusu jaribio la kushiriki udanganyifu kando na zile 30 zilizotajwa na Baraza la Kitafa la Mitihani nchini (KNEC).

“Tunachunguza shule nyingine kando na ile orodha tuliyopata kutoka Knec na baadhi ya walimu wakuu wa shule hizo. Mara hii yeyeote atakayepatikana anashiriki wizi wa mtihani atakamatwa na kama ni mwanafunzi hataweza kuendelea na wake,” akaongeza Bi Mohamed

You can share this post!

Familia ya Sharon yahitaji Sh1.3m kugharamia mazishi

UDIKTETA AFRIKA: Marais waliokatalia madarakani

adminleo