• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 8:55 AM
Ajabu ya gazeti la taifa kuchapisha habari kwa Kichina

Ajabu ya gazeti la taifa kuchapisha habari kwa Kichina

Na MASHIRIKA

LUSAKA, ZAMBIA

GAZETI la Times of Zambia linalomilikiwa na taifa hilo, limeshangaza wengi baada ya kuchapisha taarifa ya habari kwa Kichina huku ushawishi wa Uchina ukizidi kuenea nchini humo.

Taarifa hiyo ya habari ilihusu jinsi Rais Edgar Lungu, alivyosema kwamba Zambia haitapendelea mataifa ya Mashariki wala Magharibi bali itasonga mbele na yeyote yule aliyejitolea kushirikiana na nchi hiyo.

Alikuwa ametoa matamshi hayo wakati alipokutana na wajumbe wa Uswisi katika Ikulu mnamo Jumatatu.

Msemaji wa serikali, Dora Siliya, alisema hatua ya kuchapisha habari kwa Kichina inalenga kutafutia gazeti hilo soko kwa jamii ya Wachina.

Hata hivyo, hisia tofauti ziliibuka huku baadhi ya wananchi wakisema ingekuwa vyema zaidi kama habari zingechapishwa Kihindi ikizingatiwa kuna Wahindi wengi nchini humo.

Wengine walishangaa kwa nini lugha za kigeni zinachukuliwa kwa umuhimu zaidi kuliko lugha za jamii asili za Zambia.

Hivi majuzi serikali ilijitetea dhidi ya malalamishi kwamba ilitumia mali za umma kama dhamana ya mikopo mikubwa kutoka Uchina ikiwemo uwanja wa ndege wa kimataifa na shirika la habari la taifa.

-Imekusanywa na Valentine Obara

You can share this post!

UDIKTETA AFRIKA: Marais waliokatalia madarakani

Alfred Keter na wenzake wamtaka Uhuru kuhakikisha wakulima...

adminleo