• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 1:08 PM
Alama ya D+ ni ya chini mno kufuzu vyuoni – Wabunge

Alama ya D+ ni ya chini mno kufuzu vyuoni – Wabunge

Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wamepinga mpango wa serikali wa kushusha gredi ya kuwasajili wakufunzi watakaoteuliwa kujiunga na Vyuo vya Mafunzo ya Ualimu Nchini (TTCs), shughuli ambayo awamu yake ya pili ingeanza mwezi Oktoba.
Wanachama wa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu inayooongozwa na Mbunge wa Tinderet Julius Melly Jumatano walisema pendekezo la Mamlaka ya Kitaifa ya Uhitimu (Kenya National Qualification Authority, KNQA) ya kupunguza gredi  ya chini hitajika kutoka C- hadi D+ katika matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE)  utachangia kushuka kwa viwango vya elimu nchini.
Tume ya Kuajiri Walimu Nchini (TSC) pia imekuwa akipinga hatua hiyo ya KNQA ikisema itapelekea wakufunzi wengi kufeli kupita mitihani katika vyuo vya TTCs

Mnamo Juni mwaka huu KNQA, kupitia tangazo katika gazeti rasmi ya serikali ilipendekeza kuwa wakufunzi wanaopania kusomea  shahada ya diploma wawe wamepata angalau  gredi ya C- katika KCSE na wale ambao watasomea astashahada (cerficate) wawe wanapata angalau gredi ya D.

Jumatano Kamati hiyo iliwataka Waziri wa Elimu Amina Mohamed na Katibu wa Wizara hiyo Belio Kipsang kutayarisha taarifa ya kisera kuhusu suala hilo kisha waisalishe kwa kamati hiyo kwa uchanguzi.

“Sio sawa kwa gredi ya kuwasajili wakufunzi katika Vyuo vya Mafunzo ya Walimu kushushwa kiasi hiki kwani matokea yake ni kwamba taifa hilo litakuwa na walimu wenye uhitimu wa chini.

Tunataka wizara na Mamlaka ya KNQA kuandaa taarifa kuhusu suala hili na kuiwasilisha kwa kamati hii.  Tunahisi kuwa hatua hii ilichukuliwa pasina mashauriano kufanywa ndio maana TSC inapinga,” akasema Bw Melly.

Kauli yake iliungwa mkono na Mbunge wa Kipipiri Amos Kimunya aliyesema taifa hili linapasa kulenga kupandisha gredi hitaji kuwasajili wakufunzi katika vyuo vya elimu wala sio kushukisha.

“Tunafaa kuonekana kusonga mbele wala sio kurudi nyumba katika nyanja ya masomo. Walimu wenye gredi duni bila shaka hawataweza kuwafundisha watoto wetu katika kiwango ambacho kitawawezesha kushindana na wanafunzi wengine duniani,” akasema Bw Kimunya ambaye pia ndiye naibu mwenyekiti wa kamati hiyo.

Bi Mohamed na Bw Kipsang’ walitetea hatua ya KNQA kupunguza gredi hiyo wakisema itawawezesha wanafunzi waliosomea katika shule zilizoko katika maeneo yenye ugumu wa maisha kama vile Kaskazini Mashariki mwa nchi, kupata nafasi katika vyuo vya mafunzo ya ualimu.

“Mwanafunzi aliyepata alama ya D katika shule zinazopatikana maeneo kame ya kaskazini mwaka Kenya ni mwanafunzi mwerevu ambaye anaweza kulinganishwa mwenzake aliyepata gredi ya B katika kama Nairobi na kati mwa nchi. Kwa hivyo, kwa mtizamo wetu kama wizara tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na KNQA,” akasema Dkt Mohamed.

You can share this post!

Raia wa Zimbabwe pabaya kwa kuiba mali ya Oilibya

Mmiliki wa basi lililoua watu 55 ndani

adminleo