• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
Canada nayo pia yahalalisha matumizi ya bangi

Canada nayo pia yahalalisha matumizi ya bangi

BBC na PETER MBURU

CANADA imekuwa taifa la pili ulimwenguni kuhalalisha matumizi ya bangi, kwa misingi ya kimatibabu.

Hii ni baada ya taifa hilo Jumatano usiku, baada ya mjadala wa muda mrefu kuhusu masuala ya afya, sheria na usalama wa binadamu kutangaza kuwa watu wanaweza kuitumia bangi, japo kwa ajili ya matibabu.

Lakini kupitishwa kwa sheria hiyo kulikuja baada ya serikali kufahamisha kupitia jumbe familia 15milioni, zikieleza sheria mpya za matumizi ya bangi, na kufanyika kwa kampeni za kuhamasisha umma.

Mikoa na himaya tofauti sasa zitajukumiwa kutoa habari kwa umma kuhusu mahali watu wataweza kununua na kutumia bangi katika maeneo yao.

Lakini baadhi ya wachanganuzi nchini humo tayari wameonya kuwa kutashuhudiwa upungufu wa bidhaa hiyo, katika kipindi cha mwaka tu wa kufanywa sheria.

Watumizi wa bangi watakuwa na nafasi hata kufanya manunuzi kupitia njia za mitandao, haswa katika mkoa wa Ontario ambao una watu wengi zaidi.

Watu wazima wataweza kununua mafuta ya bangi, mbegu na matawi pamoja na bangi iliyokaushwa kutoka kwa wazalishaji na wauzaji waliopewa leseni. Mtu ataruhusiwa kumiliki hadi gramu 30 kwa mara moja akiwa mbele ya umma.

Katika kipindi cha mwaka, mswada wa kuanza kuuza vyakula vyenye bangi ndani yake utawasilishwa kujadiliwa ili iwe sheria.

Baadhi ya jinai zitakazokuwa katika biashara hiyo ni mtu kumiliki zaidi ya gramu 30 za bangi akiwa mbele ya umma, kupanda zaidi ya mimea minne katika boma moja na kununua bidhaa hiyo kutoka kwa mtu asiye na leseni.

Atakayepatikana akiuza bidhaa hiyo kwa mtoto wa chini ya umri wa miaka 18 atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 14. Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wamesema adhabu hiyo ni kali mno.

Canada linakuwa taifa la pili kuhalalisha matumizi ya bangi baada ya Uruguay.

You can share this post!

Uhuru apiga marufuku samaki kutoka Uchina

Kipchoge na Chepkoech watawazwa wanamichezo bora Septemba...

adminleo