Mmiliki wa Zuku kuaga soko la Kenya
Na BERNARDINE MUTANU
Mmiliki wa Zuku, Wananchi Group, amepanga kuondoka soko la Kenya baada ya kuhudumu kwa takriban miongo miwili.
Kulingana na Bloomberg, kampuni hiyo ilitoa kandarasi kwa kampuni ya Lazard kubuni mkakati wa kuuza kampuni hiyo.
Hii ni kutokana na kuwa wawekezaji wakuu, ambao wanamiliki asilimia 85 ya hisa, wamepanga kuondoka kutokana na mgogoro wa ushuru kati ya kampuni hiyo na Mamlaka ya Utozaji Ushuru nchini (KRA).
Kulingana na ripoti, wawekezaji watatu, Liberty Global, Altice Europe NV na Helios Investment Partners wanalenga kuuza hisa zao za thamani ya (Sh50 bilion) ikiwemo ni pamoja na madeni.
Wananchi inalenga watu wa hadhi ya wastani katika eneo la Afrika chini ya ukanda wa Sahara.
Lakini kampuni hiyo inaendelea kushuhudia ushindani mkubwa kutoka kwa kampuni za mawasiliano ya simu nchini.