• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Wario na wenzake wakamatwa

Wario na wenzake wakamatwa

Na GEOFFREY ANENE

WAZIRI wa Michezo wa zamani wa Kenya, Hassan Wario, amekamatwa Oktoba 18, 2018 kwa tuhuma za kuhusika katika sakata ambayo mamilioni ya shilingi za Kenya, zilizotengewa timu ya taifa ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2016, zilipotea.

Wario, ambaye wakati huu ni Balozi wa Kenya nchini Austria, alitiwa nguvuni pamoja na Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Olimpiki ya Kenya (NOC-K) Kipchoge Keino na maafisa wengine wawili baada ya kujiwasilisha katika Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) mapema Oktoba 18. Mapema juma hili mahakama iliamuru Wario arejee nchini Oktoba 18 kutoka Austria kuandikisha taarifa yake kuhusu sakata hiyo.

Maafisa hawa watashtakiwa kwa kufanya malipo ambayo hayakuidhinishwa, kulipa zaidi ya kiasi cha fedha zilizotakikana pamoja na kununua tiketi za ndege ambazo hazikutumiwa na kikosi cha timu ya Kenya, bali watu ambao hawakustahili kuwa katika safari hiyo ya Rio de Janeiro nchini Brazil.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji zinasema kwamba anaamini kuna ushahidi wa kutosha kufungulia maafisa hao mashtaka ya matumizi mabaya ya fedha. Wario atafikishwa mbele ya mahakama Ijumaa.

You can share this post!

AWCON: Safari ya #HarambeeStarlets kutinga fainali Accra

SHERIA ZA MICHUKI: Maelfu ya magari kuondolewa barabarani

adminleo