• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 10:55 AM
Two Rivers yatajwa makao makuu ya Samsung barani Afrika

Two Rivers yatajwa makao makuu ya Samsung barani Afrika

Na BERNARDINE MUTANU

KAMPUNI ya kutengeneza simu ya Samsung imefungua duka kubwa zaidi barani Afrika katika jumba la Two Rivers, kaunti ya Nairobi.

Kulingana na rais wa Samsung Sung Yoon, hatua hiyo ilikuwa ni katika sehemu ya mikakati yake ya kulainisha operesheni zake za kibiashara Afrika kwa lengo la kuimarisha ufanisi wake katika mauzo na huduma zake kwa wateja.

“Tumejitolea kutoa bidhaa zenye ubora wa juu na suluhu ya kiteknolojia kwa wateja wetu kwa njia wanayoweza kupata kwa urahisi.

“Wateja wana maazimio na wanachotaka kutoka kwa bidhaa zetu. Kufunguliwa kwa duka hilo kutawapa wateja huduma wanayohitaji,” alisema.

Duka hilo litauza bidhaa za kielektroniki na simu na pia kitakuwa ni kituo cha kutoa huduma kwa wateja.

Kufikia sasa, Samsung ina maduka 29 nchini- Nairobi, Kisumu, Mombasa, Meru, Nakuru, Thika na Kitengela.

You can share this post!

Wakazi wa Nairobi kutozwa ushuru zaidi

Hatima ya Obado, Oyamo, Obiero, Jacque na Jowie

adminleo