• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Walia marufuku ya ukataji miti imeathiri sekta ya samani

Walia marufuku ya ukataji miti imeathiri sekta ya samani

Na BERNARDINE MUTANU

Marufuku ya ukataji miti yamepelekea kupanda kwa mbao kwa asilimia 36.18. Kutokana na hilo, bei ya samani pia imepanda kwa asilimia 11.73 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kulingana na ripoti ya Shirika la Kitaifa la Takwimu nchini (KNBS), ukosefu wa mbao ulikabili wakataji miti, hali iliyowafanya kushindwa kuwatimizia mahitaji wajenzi, maseremala na watengenezaji wa bidhaa za mbao.

Katika muda wa miezi mitatu iliyopita, bei ya mbao ilipanda kwa asilimia 24.

Mwenyekiti wa Chama cha Watengenezaji wa Bidhaa za Mbao Hitesh Mediratta, hata hivyo alisema bei ya mbao iliyoongezeka ni bandia.

Alisema hilo limechochea ununuzi wa samani iliyokamilika kwa sababu samani inayotengenezewa humu nchini ni ghali sana.

“Tunahitaji marufuku ya ukataji wa miti iondolewe na kudhibiti jinsi ya kuvuna miti kwa lengo la kuwawezesha watengenezaji wa mbao kuanza tena operesheni zao. Hii ni kwa lengo la kuzindua tena sekta ya utengenezaji wa fanicha na uuzaji wa mbao ili kupunguza bei ya mbao hadi bei ya kawaida,” alisema.

You can share this post!

JAMAL KHASHOGGI: Trump aionya Saudia kwa kuficha ukweli wa...

Maafisa wa Kenya Power mashakani kuhusu kupotea kwa ushahidi

adminleo