• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 8:50 AM
Safaricom iliunda nafasi za ajira zaidi ya 800,000 – Ripoti

Safaricom iliunda nafasi za ajira zaidi ya 800,000 – Ripoti

Na BERNARDINE MUTANU

Bado kamupuni ya Safaricom inaongoza miongoni mwa kampuni zinazoshikilia uchumi wa Kenya.

Kulingana na ripoti ya hivi punde, kampuni ya Safaricom iliunda nafasi 897,372 za kazi, moja kwa moja au vinginevyo.

Katika mwaka uliokamilika Machi 2018, mchango wa Safaricom katika uchumi wa Kenya ulikuwa ni Sh57 bilioni zaidi hadi Sh543 bilioni, kulingana ripoti ya kila mwaka kuhusu maendeleo ya kampuni hiyo.

Huo ni mchango wa asilimia 6.5 kwa uchumi wa jumla wa Kenya.

Hii ni licha ya kampuni nyingi kuonekana kulemewa kiuchumi katika kipindi hicho hasa kutokana na hali ya kisiasa iliyokuwa ikishuhudiwa nchini.

Kampuni nyingi zilifuta wafanyikazi na zingine kusimamisha kuajiri kutokana na kupungua kwa mapato.

Kulingana na Safaricom, imetoa nafasi za kazi kwa watu 171,369 moja kwa moja, na wale wengine wamepata kazi kutokana na huduma na bidhaa ambazo hutolewa na Safaricom.

Kufikia Machi 2018, Safaricom ilikuwa imeajiri watu 5,556 moja kwa moja ambao iliwalipa Sh10.23 bilioni kama mishahara, bonsai, pensheni na tuzo.

You can share this post!

Yathibitishwa gesi iliyopatikana Nyeri ni CO2

Qatar yaondolea Wakenya baadhi ya vikwazo vya usafiri

adminleo