Habari Mseto

Mtambue Brigedia Vincent Naisho Loonena

November 15th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Rais Uhuru Kenyatta amemteua Brigedia Vincent Naisho Loonena kama Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Ulinzi wa Pwani ya Kenya.

Loonena atakuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu na anachukua nafasi hiyo baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 20  katika jeshi la majini.

Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa Meneja Mkurugenzi wa Mpango wa Bima wa jeshi kwa miezi minne.

Huduma hiyo itazinduliwa rasmi na Rais Jumatatu, Novemba 19, 2018 eneo la Liwatoni, Mombasa.

Huduma hiyo ilizinduliwa kuambatana na Sheria ya Huduma ya Ulinzi wa Pwani 2018 ambayo ilianza kutekelezwa Oktoba 22, 2018 ilipochapishwa katika gazeti rasmi.

Kuambatana na sheria hiyo, kutakuwa na Tume ya Huduma ya Ulinzi wa Pwani ambayo itasimamia huduma hiyo.

Mwenyekiti wa tume hiyo atakuwa ni Waziri wa Usalama na Masuala ya Ndani Dkt Fred Matiang’i na itajumuisha mawaziri wengine wakiwemo Raychelle Omamo (ulinzi), Keriako Tobiko (Mazingira na Misitu) na James Macharia (Uchukuzi, Muundo Msingi, Nyumba na Maendeleo ya Miji).