• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:55 AM
Kenya yaipongeza Uchina kuendeleza marufuku ya pembe za kifaru

Kenya yaipongeza Uchina kuendeleza marufuku ya pembe za kifaru

Na BERNARDINE MUTANU

Serikali ya Kenya imepongeza serikali ya Uchina kwa kubatilisha uamuzi wake wa awali wa kuondoa marufuku ya biashara ya pembe za kifaru na ngozi ya chui.

Serikali ya China ilibatilisha uamuzi huo Jumatatu Novemba 12 kupitia kwa Baraza la Serikali.

“Serikali na raia wa Kenya wanapongeza China kwa kutathmini uamuzi wake wa Oktoba 29, 2018 ambao ungepelekea kuondolewa kwa marafuku ya uagizaji na uuzaji, usafirishaji na uwasilishaji wa sehemu za vifaru na chui,” ilisema Wizara ya Utalii katika taarifa.

China ilikuwa imeondoa marufuku hayo ya miaka 25 kwa kusema sehemu hizo ni muhimu katika utengenezaji wa dawa.

“Marafuku hayo ni hatua nzuri kwa sababu ni muhimu kwa uhifadhi wa wanyama walio katika hatari. Katika muda wa miaka 25 ambapo marufuku hayo yamekuwa, idadi ya aina za wanyama hao imeongezeka,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliana katika Wizara ya Utalii Bw Mulei Muia katika taarifa hiyo.

Kulingana na wizara hiyo, serikali imejitolea kufanya kazi na serikali ya China kuhifadhi na kulinda wanyama na rasilimali ya porini.

You can share this post!

Kenya kuondolea Uchina vikwazo vya kibiashara

KCB yasema ongezeko la faida ni kutokana na usimamizi bora

adminleo