Kimataifa

Sayari mpya yapatikana karibu na jua

November 16th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

MASHIRIKA na PETER MBURU

WANASAYANSI wamegundua uwepo wa sayari mpya katika mfumo wa jua, ambayo inazunguka kwa karibu sana na nyota, pamoja na jua.

Sayari hiyo inasemekana kuwa na ukubwa mara tatu ya ule wa dunia, utafiti huo sasa ukitoa ishara kuwa kuna uwezekano wa uwepo wa sayari zingine ambazo bado hazijaonekana kutoka duniani huko angani.

“Tunafikiri kwamba hizi ndizo sababu ambazo zinatoa sifa na kuna uwezekano kwamba sayari nyingi za miamba ziko juu ya anga,” akasema mwanasayansi Guillem Anglada Escudé.

Sayari hiyo inasemekana kuwa na wingi wa mvuke unaotokana na maji, gesi ukaa na vitu vingine na kuwa imekaribiana na jua.

Sayari ya nyota ya Barnard iko mbali na nyota kama lilivyo jua na sayari ya Mekuri.

Hii ni sayari ambayo iko karibu na dunia baada ya Proxima ambayo ilitangazwa kugundulika mwaka 2016.

Nyota ya Bernard haina mwanga wa kutosha, kwani mwanga wake unakadiriwa kuwa thuluthi moja ule wa jua.

Wanasayansi hao hata hivyo walisema kuwa bado wanaendeleza utafiti wao ili kuwa na uhakika wa kutosha kuhusiana na suala hilo.

“Tunaweza kufanya jaribio moja ambalo linaweza kubaini utofauti wake, hivyo tutajumuisha taarifa zote kwa makini. Tumebaini kuwa kuna makosa mengi yanayotokana na vifaa mbalimbali ambavyo vilitumika. Hii haimaniishi kuwa tunalenga kupata takwimu mpya lakini tunataka watu waelewe namna ambavyo mfumo unaathirika,” akasema Mhadhiri mmoja kutoka chuo kikuu cha Queen Mary, Uingereza.

Wanasayansi hao, hata hivyo, walieleza kuna uwezekano vizazi vijavyo vitazidi kugundua sayari nyingine nyingi ambazo kwa sasa hazionekani kutoka hapa duniani.

Si mara ya kwanza wanasayansi kudai wameona sayari nyingine angani kwani mnamo 1960, mwanasayansi Peter van de Kamp kutoka Marekani alichapisha kuhusu ushahidi wa nyota hiyo.