• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:12 PM
Wakili Mholanzi anayeshtakiwa kubaka wasichana atupwa rumande

Wakili Mholanzi anayeshtakiwa kubaka wasichana atupwa rumande

Na RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Uholanzi aliyefikishwa mahakamani Ijumaa kujibu mashtaka ya kuwabaka wasichana wa umri mdogo aliokuwa anafadhili elimu yao alinyimwa dhamana..

Bw Hans Egon Dieter, wakili aliyestaafu mwenye umri wa miaka 66 alikana mashtaka mawili ya kuwabaka na kuwalawiti wasichana wenye umri wa miaka minane na kumi katika makazi yake mtaa wa Roysambu Nairobi miaka minne iliyopita.

Raia huyo wa kigeni mwenye hari ya kuwadhulumu wasichana kimapenzi aliamriwa azuiliwe gerezani hadi Novemba 16 mwaka huu wakati walalamishi watakapofika mahakamani kutoa ushahidi.

Bw Dieter alinyimwa dhamana na hakimu mkazi mahakama ya Milimani Bi Caroline Muthoni Nzibe.

Bi Nzibe alisema polisi wanahitaji kupewa muda kutengeneza nakala za mashahidi na kumkabidhi mshtakiwa ndipo aandae tetezi zake.

Mahakama iliamuru kesi hiyo itajwe Novemba 23, 2018 ndipo polisi waeleze ikiwa mshhtakiwa amepwa nakala za mashahidi.

Kiongozi  wa mashtaka Bi Edna Ntabo alipinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana akisema “kwa muda wa miaka miwili alikuwa ametoroka na polisi wamekuwa wakimsaka.”

Pia alisema mshtakiwa atawavuruga mashahidi kwa vile wengi wao ni wale huwasaidia katika shule yake ya kibinafsi iliyoko eneo la Kiusyani , kaunti ya Kitui.

Mbali na kuwabaka wasichana hao mshtakiwa alikuwa akiwapiga picha akiwatendea unyama huo wa kuwabaka na kuwalawiti.

Mshtakiwa aliamriwa azuiliwe katika gereza la Viwandani, Nairobi akisubiri maagizo zaidi kuhusu dhamana.

You can share this post!

Kipchoge aponyoka kesi ya ufisadi

Nusu ya watahiniwa wa ualimu wafeli vyuoni

adminleo