• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 12:48 PM
FUNGUKA: ‘Tunavyosisimua ladha chumbani…’

FUNGUKA: ‘Tunavyosisimua ladha chumbani…’

NA PAULINE ONGAJI

KATIKA jamii nyingi, ndoa hasa huhusisha mwanamume mmoja na mwanamke mmoja. Aidha kuna jamii zingine ambazo zimemruhusu mwanamume kuwa na zaidi ya mke mmoja na wala sio mke kuwa na waume kadha.

Lakini Kwa Betty, 35, Kevin, 45, na Derrick, 37, mambo ni tofauti. Watatu hawa wana uhusiano ambao jamii nyingi zitakunja uso kusikia upo. Betty na Kevin wamekuwa katika ndoa kwa zaidi ya miaka kumi na pamoja wamejaliwa watoto wawili. Lakini miaka mitano iliyopita wawili hawa waliamua kwamba uhusiano wao kidogo umechuja, hauna ule msisimko na hivyo wakaamua kuongeza ladha.

Ladha hii kwao ilimaanisha kumshirikisha mhusika mwingine katika uhusiano huu. Derrick ndiye aliyeongezwa kuchangamsha ndoa hii ambapo Betty anasimulia uhusiano huu usio wa kawaida machoni mwa wengi.

“Nilikutana na Derrick katika sherehe moja ambapo niligundua uzuri wake baada ya kumbusu mara ya kwanza. Nakumbuka jinsi nilivyohisi mwunganisho na kutokana na sababu kwamba sikutaka kumlaghai mume wangu, niliamua kumpendekezea wazo la kumuongeza katika uhusiano wetu.

Mume wangu alifurahia wazo hili na baada ya kukutana na Derrick, basi tukakata kauli.

Anaishi nasi na sote tunalala katika chumba na hata kitanda kimoja na kwa kawaida ni mimi hulala katikati. Tumemhusisha katika kila jambo kwenye ndoa yetu ikiwa ni pamoja na malezi ya watoto wetu.

Katika masuala ya mahaba kuna wakati ambapo sote hujumuika pamoja kwa wakati mmoja, lakini mara nyingi kila dume ana zamu yake nami.

Derrick anafanya kazi kama mwanasarakasi ambapo mimi ni msaidizi wake. Kwa hivyo tukiwa kazini, Kevin anasalia na watoto na kuwashughulikia. Kwa upande mwingine kutokana na sababu kwamba ajira ya Kevin inamlazimu kusafiri kila wakati, akiwa katika shughuli zake, basi ni sisi husalia na watoto.

Hata watoto wetu wamezoea maisha haya na wanajua kwamba wana baba wawili na mama mmoja.

Najua kuna wanaoshangaa tunavyofaulu kufanya hivyo ilhali twajua wivu ni jambo la kawaida kati ya wapendanao? Mwanzo kabisa, tunaelewana na japo ni kawaida wivu kujitokeza, tunazo mbinu za kukabiliana na changamoto hii kama vile kuzungumzia pindi tatizo linapozuka.

Aidha ili Kevin asihisi kana kwamba hapati haki yake kamili, tumekubaliana awe na mpenzi wake wa kando na wamekuwa wapenzi kwa mwaka mmoja sasa na bibi huyu anajua kuhusu mpangilio wa familia yetu.

Anaruhusiwa kushiriki mahaba naye mradi tu asimshirikishe katika masuala ya kifamilia.

Wazazi wangu hawafurahishwi na mpango wetu lakini mamake Kevin hana noma nasi mradi tuna furaha”.

You can share this post!

Dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake zachacha Sudan Kusini

FKF yahamisha kambi ya Harambee Stars kutoka Ufaransa hadi...

adminleo