• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
AKILIMALI: Uundaji kamba kwa nyavu za samaki wawapa umaarufu na kipato

AKILIMALI: Uundaji kamba kwa nyavu za samaki wawapa umaarufu na kipato

Na STEPHEN DIK

Bi Josephine Anyango na msaidiza wake, Bi Monica Akoth ni wasusi wa kamba ndefu za kufunga mifugo, kamba hizi wanatengeneza kwa kutumia nyavu za kuvua samaki.

Ukifika mjini Bumala kaunti ya Busia na kusema wataka mama kamba, basi bila shaka utapelekwa hadi kwa Bi Josephine.

Mama huyo anasema kazi hii ameifanya kwa takriban miaka nane, na kwamba alifunzwa na mfanyabiashara mwenzake. Josephine anasema kuwa yeye husafiri hadi kwa ufuo wa Ziwa Victoria ambapo anapata wavuvi wengi na kununua nyavu zilizoharibika. Amekuwa akisafiri kwa ufuo unaojulikana kama Mageta Beach huko kaunti ya Siaya na kununua nyavu moja kwa Sh1,000. Nyavu hizo huuzwa na wavuvi waliobadilisha nyavu zao wanazotumia kwasababu zimeharibika, na kuweka zingine mpya.

”Nyavu ambazo mimi nanunua kwa wavuvi ni zile haziwezi kutumika katika uvuvi kwasababu zimetoboka au kuzeeka,” anasema Bi Josephine. ? Wakati amenunua nyavu hizo huwa anazichambua, anasema anazichambua kwasababu nyuzi huwa zimechanganyika kubwa na ndogo.

Kwanza, anadokeza kuwa yeye hutoa nyuzi pana na kuweka kando, kisha nyuzi ndefu nyembamba ndio anaziunganisha na kutumia kusuka au kusokota kamba kubwa za kufunga wanyama.

Kamba ambazo anasuka ndio hutumika kwa kufunga mifugo na wateja huzipenda kwa sababu huwa hazikatiki kwa urahisi. Wateja wamekuwa wakizisifia kamba hizo wakisema zinadumu muda mrefu kuliko zile kamba za makonge.

Wakati wa msimu wa mvua ambapo watu wamepanda mimea ndio biashara ya Bi Josephine huwa imenoga.? Wateja wengi hununua kamba hizo ili kufunga mifugo yao isiharibu mimea ya wenyewe shambani.

Anasema kuwa yeye husuka kamba zaidi ya kumi kwa siku moja na kuziuza zote kwa Sh150 kila moja.? Amekuwa akipata zaidi ya Sh2,000 kwa siku kazi ambayo anasema ni bora kuliko ile alikuwa akifanya ya kuuza vitunguu.? Bi Josephine anasema kuwa kazi ya kuuza vitunguu ambayo alikuwa akifanya mwanzoni ilikuwa ya mapato duni ikilinganishwa na hii.

You can share this post!

AKILIMALI: Teknolojia yamwezesha kuangua watoto wa samaki...

AKILIMALI: Spinachi ya majani makubwa inayovunwa miaka 2...

adminleo