TAIFA LEO Logo
  • Habari
    • Habari za Kitaifa
    • Habari za Kaunti
    • Kimataifa
  • Siasa
  • Maoni
  • Makala
    • Afya na Jamii
    • Lugha, Fasihi na Elimu
    • Akili Mali
    • Jamvi La Siasa
    • Shangazi Akujibu
    • Bambika
    • Pambo
    • Dimba
  • Dondoo
  • Bi Taifa
  • Mashairi
  • Michezo
  • NIE Shuleni
Habari Mseto

Chungeni msilipukiwe na gesi, Kuria aonya polisi Kiandutu

February 3rd, 2024 Kusoma ni dakika: 1
  • Shiriki mitandao ya kijamii:
  • Facebook
  • X
  • LinkedIn
  • Email
  • WhatsApp

NA MWANGI MUIRURI

WAZIRI wa Utendakazi wa Umma Moses Kuria amedai kwamba kuna kiwanda haramu cha gesi katika Kaunti ya Kiambu kinachohudumu karibu na kituo cha polisi.

Amedai kwamba kiwanda hicho alichosema kiko katika mtaa wa Kiandutu, kiko katika hatari ya kulipuka kwa wakati wowote na walio katika hatari kuu, ni maafisa wa polisi walio na afisi zao hapo karibu.

Aliongeza kwamba kituo hicho cha gesi hakina usajili wowote wa kisheria na kwamba ni haramu, ni hatari na hivyo kinafaa kuhalalishwa au kufungwa.

Soma Pia: Embakasi: Nema yatimua maafisa wanne kwa kutoa leseni tata

Wenyeji katika mtaa huo wa viunga vya mji wa Thika waliambia Taifa Leo kwamba kiwanda hicho huambatana na ukora mwingi sana hata wa kushambuliana kwa bunduki.

“Ni kiwanda cha kipekee. Mara kwa mara huwa kunazuka vita vya ufyatuliamaji risasi katika barabara ya kuingia na kutoka kiwandani humo,” akasema jirani wa kiwanda hicho.

Kiwanda cha gesi cha Kiandutu ambacho Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria amekimulika. PICHA | MWANGI MUIRURI

Hayo yanajiri huku Rais William Ruto akitoa msimamo mkali dhidi ya mamlaka za kutoa leseni kwamba wote watakaonaswa katika mtandao wa ufisadi, utepetevu na uzembe unaohatarisha maisha ya watu, watakamatwa, wafutwe kazi na kutupwa jela.

Hii ni baada ya kiwanda katika mtaa wa Embakasi kulipuka na kusababisha vifo vya watu watatu huku zaidi ya 300 wakipata majeraha.

[email protected]

Mfanyakazi wa Khalwale kuzikwa Jumatatu
  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Email
  • WhatsApp
Maiti ya kitoto malaika yatupwa karibu na ofisi ya umma

Habari Mseto Zaidi

Wenye majengo jijini wapewa siku 14 kuyapaka rangi lau...

October 7th, 2025

Mpango wa mbolea ya bei nafuu umetekwa na wakora, EACC sasa...

October 6th, 2025

Afueni kwa wahanga wa uvamizi wa mamba Tana River mradi wa...

October 3rd, 2025

Wakenya waumia huku serikali ikisema hali ni shwari,...

September 26th, 2025

Habari Za Sasa

Jaji alivyomnyima Raburu mamilioni ya Bazu

October 11th, 2025

Tumewasajili wapiga kura 20,754 pekee kufikia Oktoba 8,...

October 11th, 2025

Biya, 92, aahidi Gen Z wa Cameroon mazuri akishinda muhula...

October 11th, 2025

Jinsi dawa ya kikohozi ilivyosababisha vifo vya watoto India

October 11th, 2025

KenyaBuzz

One Battle After Another

When their evil nemesis resurfaces after 16 years, a band...

BUY TICKET

The Long Walk

In a dystopian, alternate-America ruled by a totalitarian...

BUY TICKET

Code 3

A burned-out paramedic tries to survive his last 24 hours...

BUY TICKET

A CELEBRATION OF OPERA

It is World Opera Day!!!!! Come celebrate World Opera...

BUY TICKET

CAROLS IN BRASS CONCERT

Experience the wonder of the season in sound by The Kenya...

BUY TICKET

Better Life Dinner Dance

BUY TICKET
TAIFA LEO Logo

Mitandao ya kijamii

Maarufu sana

Mwanamume ahukumiwa kifo kwa ‘kumkosoa’ rais kwenye Facebook

October 4th, 2025

Nassir: Niligutushwa na simu ya Raila kwamba hafla ya ODM imeahirishwa

October 6th, 2025

IEBC imeandikisha wapiga kura wapya 7,048 tu kwa siku sita

October 4th, 2025

Usikose

Jaji alivyomnyima Raburu mamilioni ya Bazu

October 11th, 2025

Tumewasajili wapiga kura 20,754 pekee kufikia Oktoba 8, 2025-Ethekon

October 11th, 2025

Biya, 92, aahidi Gen Z wa Cameroon mazuri akishinda muhula wa nane

October 11th, 2025
Copyright © 2025 Nation Media Group. All rights reserved.