• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:45 AM
Polisi kutumia ‘Alcoblow’ mchana kunasa walevi msimu wa Krismasi

Polisi kutumia ‘Alcoblow’ mchana kunasa walevi msimu wa Krismasi

Na Peter Mburu

POLISI sasa wataanza kuwawinda madereva wanaolewa majira ya asubuhi na kuendesha magari, kama njia moja ya kuzuia ajali nyingi za barabarani msimu huu wa Krismasi.

Inspekta Jenerali wa Polisi Joseph Boinnet jana aliwatahadharisha madereva wasio na maadili kuwa sasa chuma chao ki motoni, kwani polisi wa kupima ulevi wa madereva watakuwa barabarani saa zote.

“Tumeamua kubadili mbinu, kwa wale ambao wamezoea kutupata tukipima ulevi usiku sasa watutarajie kufanya kazi hiyo saa tofauti,” alisema Bw Boinet jana.

Bw Boinet alisema baadhi ya madereva wana tabia ya kulewa kupita kiasi usiku, na kuwa wanapofika kazini asubuhi huwa bado ni walevi.

Alisema utundu huo wa madereva sharti ukomeshwe ili kuhakikishia Wakenya wanaosafiri kuelekea sehemu tofauti za nchi usalama wao.“Ukijua siku inayofuata utaendesha gari, kunywa kwa ustaarabu ama usikunywe. Lazima tukomeshe utundu ambao husababisha mauti,” akasema Bw Boinnet.

Alikuwa akizungumza afisini mwake, Nairobi.

 

You can share this post!

UFISADI: Afisa mteule EACC afichua alinolewa katika FBI na...

Wakeketaji sasa wafungua kliniki za kibinafsi kisiri

adminleo