Waziri Mkuu wa Haiti ‘ahepea’ Puerto Rico
NA MASHIRIKA
WAZIRI Mkuu wa Haiti Ariel Henry alitua Puerto Rico Jumanne jioni na hivyo kuondoa wasiwasi kuhusu aliko baada ya ziara yake nchini Kenya.
Afisi ya Gavana wa Puerto Rico ilithibitisha kuwa ndege iliyombeba kiongozi huyo ilitua katika jiji kuu San Juan.
Hii ni baada ya ripoti kadhaa za vyombo vya habari kusema Jamhuri ya Dominican, inayopakana na Haiti kupitia kisiwa cha Hispaniola, awali ilikosa kutoa kibali kwa ndege ya waziri huyo mkuu kutua hapo.
Henry alikuwa amesafiri Kenya wiki jana kutia saini mkataba wa kuruhusu taifa hilo la Afrika Mashariki kutuma polisi 1,000 nchini mwake kudhibiti usalama kwa kukabili magenge.