• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Bunge lamwidhidnisha Mbarak kuwa CEO wa EACC

Bunge lamwidhidnisha Mbarak kuwa CEO wa EACC

Na CHARLES WASONGA

Twalib Mbarak sasa ndiye atakayeshikilia wadhifa wa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kuanzia mapema mwaka ujao.

Hii ni baada ya wabunge kuidhinisha ripoti ya Kamati ya Haki na Masuala ya Sheria (JLAC) iliyoidhinisha uteuzi wake baada ya kumpiga msasa wiki jana.

Sasa jina la Bw Mbarak litawasilishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta kwa uteuzi rasmi wakati wowote kuanzia sasa.

Wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi Aden Duale na mwenzake wa Wachache John Mbadi, wabunge walimtaja Bw Mbarak kama aliyehitimu na anayefaa kwa wadhifa huo.

“Ninaunga mkono uteuzi wa Mbarak kwani amehitimu kwa kazi hiyo. Kwa hivyo, namtaka kutumia tajriba yake ya zaidi ya miaka 30 kama afisa wa kijasusi kusafisha EACC,” akasema.

Bw Duale alimtaka Mbarak kuelekeza kugatua vita dhidi ya ufisadi katika ngazi za kaunti ili kuokoa pesa za umma.

“Inasikitisha kuwa zaidi ya Sh1 trilioni zimepelekwa katika serikali za kaunti kufikia sasa lakini kiasi kikubwa cha pesa hizi zimeliwa.”

Mbaraka anafaa kuwaandama maafisa wafisadi ambao wanawakosesha wananchi huduma na miradi ya maendeleo mashinani,” akasema.

Naye Bw Mbadi alimtaka Bw Mbarak kuanza mchakato wa kuwapiga msasa wafanyakazi wote katika afisi kuu ya EACC pia atakaingia afisi.

“Tunamtaka Mbarak kuanza kwa kusafisha EACC kutoka ndani kwanza. Njia ya kipekee ya kutimiza hili ni kuwachunguza maafisa wote katika afisi yake ili kuondoa wale wenye sifa mbaya,” akasema Mbunge huyo wa Suba Kusini.

Wabunge wote waliochangia kwenye mjadala wa ripoti hiyo ya JLAC waliunga mkono uteuzi wa Mbarak wakiwataka Wakenya na asasi zingine za serikali kumuunga mkono.

You can share this post!

Pogba, De Gea na Lukaku walichochea kufutwa kwangu –...

Gavana Mutua na Keter roho mkononi wakisubiri hatima Ijumaa

adminleo