• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
KCSE: 440,000 walizoa D+ kwenda chini

KCSE: 440,000 walizoa D+ kwenda chini

Na CHARLES WASONGA

ZAIDI ya thuluthi mbili ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE) mwaka huu walifeli kupata gredi za kuwawezesha kusomea kozi za diploma.

Hii ina maana kuwa jumla ya wanafunzi 440,409 walipata gredi za D+ kwenda chini. Hii ina maana kuwa wataanzia kusomea kozi za kiwango cha astashahada (certificate) katika vyuo vya kadri.

Na wale ambao walipata gredi ya E hawatapata nafasi ya kujiunga na vyuo vya kadri ilisipokuwa vyuo anuai vya ngazi ya chini, yaani village polytechnics.

Uchanganuzi wa matokeo yaliyotangazwa Ijumaa na Waziri wa Elimu Amina Mohamed ulionyesha kuwa jumla ya wanafunzi 96,512 walipata gredi ya D+. Wale waliopata alama ya D ni 147,918, D- (165,139 na 30,840 walipata alama ya E.

Wanafunzi waliopata C walikuwa 40,707 huku 71,047 wakipata C-. Kundi hili la wanafunzi wataweza kujiunga na vyuo vya mafunzo ya kiufundi (TIVET) na vyuo vya mafunzo ya walimu (TTCs).

Mnamo Oktoba mwaka huu, Mamlaka ya Kitaifa ya Uhitumu (KNQA) ilipunguza gredi ya chini inayohitajika kwa wanafunzi kusajiliwa kusomea kozi za diploma na astashahada (certificate) katika TTCs. Ilipunguza gredi ya diploma kutoka C hadi C- na ile ya certificate ikashushwa kutoka C- hadi D+

Hatua hiyo ilipingwa na wadau, haswa Tume ya Kuajiri Walimu Nchini (TSC) na Kamati ya Bunge kuhusu Elimu. Isitoshe, mahakama ya Leba ilizima hatua hiyo ambayo iliungwa mkono na kuidhinishwa na Waziri Mohamed.

Jaji Byran Oganya alimwamuru Waziri kuitisha mkutano wa wadau haraka iwezekenavyo ili kusawazisha kujadili na kupata muafaka kuhusu suala hilo.

You can share this post!

KCSE: Matokeo ya masomo 14 yaliimarika

Sherehekeeni Krismasi bila wasiwasi, Boinnet awahakikishia...

adminleo