Ramaphosa akanusha kutumia umeme kujizolea umaarufu
NA MASHIRIKA
PRETORIA, AFRIKA KUSINI
RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Pamaphosa, amekanusha madai ya upinzani kwamba kuimarika kwa ugavi wa umeme kunatokana na uchaguzi mkuu ujao, utakaofanyika Mei 29, 2024.
Chama kikuu cha upinzani Democratic Alliance wiki iliyopita kilidai kwamba kuimarika kwa huduma za umeme kunatokana na uingiliaji wa kisiasa uliofanywa na ANC.
Kinakituhumu chama hicho tawala kwa kuiwekea shinikizo kampuni ya kusababaza umeme ya Eskom kuhakikisha umeme unapatikana.
Katika kipindi cha mwaka 2023 kiwango cha ugavi wa umeme kilifikia kilele chake na kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka huu 2024. Lakini tangu kipindi cha kampeni huduma zimerudi kuwa sawa.
Ramaphosa amesema kwamba Kuimarika kwa huduma za Eskom kunaonyesha kwamba mpango wa nishati wa serikali uliotangazwa 2022 unafanya kazi na unazaa matunda.