Iraq yashambulia kambi ya Amerika kwa roketi nchini Syria
HASAK, SYRIA
NA MASHIRIKA
ROKETI zilirushwa Jumapili jioni kutoka kaskazini mwa Iraq katika kambi ya kijeshi nchini Syria inayohifadhi muungano unaoongozwa na Amerika, kulingana na vikosi vya usalama vya Iraq.
Vikosi vya wanajeshi wa Iraq vikijibu, vilianzisha operesheni kubwa ya kusaka kaskazini mwa mkoa wa Nineveh na kupata gari lililotumiwa katika shambulio hilo, walisema katika taarifa.
Ni shambulio la kwanza kubwa dhidi ya vikosi vya muungano katika wiki kadhaa.
Hayo yanajiri siku chache baada ya Israel kuripotiwa kujibu shambulio la Iran kwa kutumia droni katika jamhuri ya Kiislamu, huku kukiwa na mvutano uliochochewa na vita Ukanda wa Gaza.
Taarifa hiyo kutoka kwa vikosi vya usalama vya Iraq ilishutumu “vita haramu kwa kulenga msingi wa muungano wa kimataifa wenye makombora katikati mwa ardhi ya Syria”, karibu saa 3.50 usiku.
Vikosi vya usalama viliteketeza gari lililohusika katika shambulio hilo, taarifa hiyo iliongeza.
Wakati huo huo, afisa wa Gaza asema kwamba shambulio la Israel limeua watu tisa wa familia moja katika eneo la Rafah
Rami Abdel Rahman, mkurugenzi wa shirika la uchunguzi wa vita vya Syrian Observatory for Human Rights, alisema makombora kadhaa yamerushwa “kutoka ardhi ya Iraq kwenye kambi ya Kharab al-Jir” kaskazini mashariki mwa Syria, ambako kuna wanajeshi wa Amerika.
Aliishutumu Islamic Resistance in Iraq, muungano legelege wa makundi yanayoungwa mkono na Iran, kwa kufanya shambulio hilo.
Kundi hilo limedai kuhusika katika mashambulizi mengi dhidi ya vikosi vya Amerika yaliyofanywa kati ya katikati ya mwezi wa Oktoba na mapema Februari.
Kufuatia msururu wa mashambulizi ya roketi na mashambulizi ya droni za makundi yanayoiunga mkono Iran dhidi ya wanajeshi wa Amerika waliotumwa Mashariki ya Kati wakati wa majira ya baridi kali, kumekuwa na wiki kadhaa za utulivu.
Kundi la Islamic Resistance lililo Iraq limesema linafanya kazi kwa mshikamano na Wapalestina na kutokana na kukasirishwa na uungaji mkono wa Amerika kwa Israel katika vita vya Gaza.
Shambulio la Januari 28 la droni liliua wanajeshi watatu wa Amerika katika jangwa la Jordan kwenye mpaka wa Syria.
Kwa kujibu, jeshi la Amerika lililenga shabaha kadhaa nchini Syria na Iraq, zikilenga vikosi vinavyoiunga mkono Iran, na kukosolewa na serikali za nchi zote mbili.
Amerika ina takriban wanajeshi 2,500 walioko Iraq na karibu 900 kwenye mpaka wa Syria kama sehemu ya muungano wa kimataifa ulioundwa mwaka 2014 kupambana na kundi la Islamic State (IS).