Habari Mseto

Wakazi wa Kisumu watahadharishwa ‘Nairobi fly’ wakitua huko kwa wingi

May 6th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA ELIZABETH OJINA

WAKAZI wa jiji la Kisumu wametakiwa kuwa macho kutokana na kuchipuka kwa uvamizi wa Narrow Bee Fly almaarufu Nairobi Fly katika maeneo ya Dunga na Paga.

Wadudu hao wanaofanana na nyuki huwa na sumu kali ambayo huchoma ngozi ya binadamu. Sumu wanayoitoa inaitwa pederin.

Kwa mujibu wa watafiti, Nairobi Fly hawaumi ila sumu yake husababisha ngozi kuvimba.

Mkugurenzi wa Afya ya Umma ya Kaunti ya Nairobi Fred Oluoch amewataka wakazi wasiue wadudu hao kwenye ngozi zao bali wawapuulize mbali ili kujilinda.

Bw Oluoch aliwataka wakazi wa Dunga na Paga wachukue tahadhari huku akisema mvua kubwa inayoendelea kushuhudiwa sasa imesababisha wadudu hao waendelee kuzaana kwa wingi na kuibua hatari.

Kwa wakulima wadudu hao ni nafuu kwa kuwa hupambana na wadudu hatari wanaoharibu mimea.