Marufuku ya magari ya kibinafsi katika Maasai Mara yaudhi wengi
NA TOBIAS MESO
UAMUZI wa serikali ya Kaunti ya Narok wa kupiga marufuku magari ya kibinafsi kuingia katika Mbuga ya Kitaifa ya Maasai Mara umezua kero miongoni mwa watalii ambao huzuru mbuga hiyo kila mara.
Kwenye taarifa aliyotoa Juni 3, 2024 , msimamizi wa mbuga hiyo Alex Nabaala alisema ni magari machache tu yataruhusiwa kuingia mbugani humo.
“Kwa mujibu wa taratibu za utekelezaji wa Mpango wa Kuimarisha Usimamizi wa Mbuga ya Maasai Mara, tumepiga marufuku matumizi ya magari ya kibinafsi kuzunguka ndani ya mbuga hiyo. Magari yatakayotumika katika shughuli hizo ni yale ya aina ya Safari trucks, Safari Land Cruisers na Safari Vans. Mnaombwa kutii agizo hili,” akasema Bw Nabaala.
Mbuga ya Maasai Mara huvutia maelfu ya watalii kila mwaka wanaofika kujionea wanyama pori kwa ukaribu.
Huchangia kiasi kikubwa cha mapato katika sekta ya utalii.
Soma Pia: Biashara yanoga Maasai Mara uhamaji wa nyumbu ukibisha