• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 1:36 PM
Wasichana wa Narok kuchunguzwa kama wamekeketwa

Wasichana wa Narok kuchunguzwa kama wamekeketwa

Na GEORGE SAYAGIE

KAMISHNA wa Kaunti ya Narok, George Natembeya (pichani kulia), amesisitiza kuwa wasichana wote wa shule katika kaunti hiyo watapimwa kuhakikisha hawana mimba na hawajakeketwa shule zikifunguliwa.

Bw Natembeya aliagiza wakuu wa shule kuhakikisha kwamba wasichana wa shule za sekondari na wanaosoma katika madarasa ya juu ya shule za msingi wanachunguzwa katika vituo vya afya.

Alisema amebuni kamati ya kuchunguza janga la mimba za wasichana wa umri mdogo ambayo itakuwa ikitembelea shule kuchunguza iwapo wamepimwa kuhakikisha hawana mimba. Kamati hiyo inashirikisha maafisa kutoka utawala wa mikoa, afya, elimu na idara ya masuala ya jinsia.

Narok inaongoza kwa mimba za wasichana wenye umri mdogo nchini huku asilimia 40 ya wasichana wakiripotiwa kuwa na mimba. Mwaka jana, wasichana 233 kutoka shule nane za sekondari na msingi waliokuwa na umri wa kati ya miaka 10 na 19 walilazimika kuacha masomo baada ya kupatikana wakiwa na mimba.

Zaidi ya wasichana 60 walikosa kufanya mitihani ya kitaifa kwa sababu ya kupata mimba. Bw Natembeya alitaja hali hiyo kuwa janga. “ Ili kuangamiza janga hili, suluhu ni kuwapima wasichana wakifungua shule kwa muhula mpya,” alisema.

BwNatembeya. Alionya kuwa wazazi ambao wasichana wao watapatikana wamekeketwa watakamatwa na kushtakiwa.

You can share this post!

Ongwae akanusha njama ya kuilaghai Serikali Sh54 milioni

Madaktari huiba dawa za wagonjwa Migori na kuziuza TZ...

adminleo