• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Mradi wa Wings to Fly kufaidi wanafunzi 1,000

Mradi wa Wings to Fly kufaidi wanafunzi 1,000

Na CHARLES WASONGA

WANAFUNZI 1000 werevu kutoka familia masikini sasa watapata nafasi ya kujiunga na shule za upili kuanzia Jumatatu baada ya kupata udhamini chini ya mpango unaendeshwa na Benki ya Equity, Wings to Fly.

Wanafunzi hao waliteuliwa miongoni mwa wanafunzi 20,000 kutoka sehemu mbalimbali humu nchini waliotuma maombi ya kutaka udhamini huo.

Akiongea wakati katika hafla ya kuwatambua rasmi wanafunzi hao waliopata matokeo mazuri katika mtihani ya darasa la nane mwaka jana, Waziri wa Elimu Amina Mohamed aliwashauri kutumia vizuri nafasi hiyo ili nao wawezi kuwasaidia wanafunzi wengine masikini miaka zijazo.

“Tafadhali msilegee…. mtie bidii masomoni ili mweze kufaulu. Kila kizazi huwa kinawajibu wa kusaidia kizazi kitakachofuatia. Sasa tunalipa madeni yetu wakati, nyie pia mtahitajika kulipa madeni yetu siku zijazo,” akasema katika ukumbi wa bewa kuu la Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako shughuli hiyo iliendeshwa Ijumaa.

Tangu kuanzishwa kwa mpango huo, wanafunzi 10,084 kutoka jamii masikini wameweza kumaliza masomo yao ya shule za upili kwa msaada wake.

Wanafunzi 8,062 miongoni mwao wamejiung na vyuo vikuu huku wengine 2,022 wakijiunga na vyuo vya kifundi kusomea kozi mbalimbali za kitaaluma.

Wanaopewa ufadhili wa masomo chini ya mpango huo wa Wings to Flya pia hupewa mafunzo ya uongozi, kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Equity James Mwangi.

Mafunzo haya huwawezesha kufanikiwa pakubwa katika kazi zao za ajira na zile za kujitegemea siku za usoni.

You can share this post!

Zimbabwe kutimua wafanyakazi 3,000 kuokoa uchumi

Mswizi aambukizwa Ebola Burundi

adminleo