Afya na Jamii

Wanafunzi 100 wa Mukuru watibiwa maradhi ya kuvuta hewa chafu

Na SAMMY KIMATU July 9th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

ZAIDI ya watoto 100 kutoka taasisi nne za elimu katika meaneo ya Mukuru walipelekwa katika Kliniki ya Mary Immaculate South B, kaunti ndogo ya starehe kwa matibabu ya magonjwa sugu yanayohusishwa na uchafuzi wa hewa.

Ripoti ya Mukuru Pomotion Center (MPC) ambayo ni mfadhili mwenza wa shule nne za msingi za umma zilizoko kaunti ndogo ya Makadara, ilionyesha kuwa kwa bahati mbaya huduma za hospitali za umma hazikupatikana kwa muda wa miezi miwili iliyopita kutokana na mgomo uliokithiri wa madaktari kote nchini.

Shule hizo ni pamoja na Sancta Maria-Mukuru, St Elizabeth, St Catherine na shule ya msingi ya St Bakhita.

Afisa wa maendeleo wa MPC, Bi Dinah Mwendwa alihoji wafanyakazi wa kijamii wamekuwa wakifuatilia kwa karibu hali hiyo, hasa kwa waathiriwa ambao walikuwa wagonjwa sugu.

Aliongeza kwamba kliniki ilitibu wagonjwa 1,525 mwezi wa Aprili, wastani wa wagonjwa 76 kwa kila siku na ilifanya vipimo vya maabara 722 ikiwa ni wastani wa vipimo 36 kwa kila siku.

“Mgomo huo umeathari pakubwa watoto wanaopokea matibabu maalum. Wameshindwa kuhudhuria masomo yao. Baadhi ya watoto watahitaji kufanyiwa vipimo vya ziada kutokana na muda mrefu bila huduma katika hospitali na hivyo kuongeza matatizo ya kifedha wazazi wasioweza kumudu gharama za ziada sababu ya umaskini,” linasema jarida la usimamizi wa MPC.

Kulingana na matokeo, baada ya vipimo 722 vya maabara kuchukuliwa, tulipata kuna wastani wa kila siku wa wagonjwa 36 waliougua. Ugonjwa wa kawaida mwezi Aprili ulikuwa matatizo ya kupumua hasa miongoni mwa watoto walio na umri chini ya miaka 5 kuwa kundi kubwa zaidi.

[email protected]