Michezo

Vipusa wa Zambia wafurushwa Olimpiki kwa kuchezesha mwanamume

Na JOHN ASHIHUNDU NA MASHIRIKA August 1st, 2024 Kusoma ni dakika: 1

TIMU ya soka ya wanawake ya Zambia imepigwa marufuku kushiriki Michezo ya Olimpiki kwa muda usiojulikana baada ya sehemu za siri za mchezaji mmoja kubainika kuwa za kiume.

Timu hiyo hata hivyo ilikuwa imeshindwa vibaya katika mechi za Kundi B ambalo pia lilijumuisha Australia, Ujerumani na Amerika.

Baada ya mechi za makundi, Ufaransa, Canada, Colombia, Amerika, Ujerumani, Uhispania, Japan na Brazil zimetinga hatua ya robo fainali.

Ufaransa walikuwa katika Kundi A pamoja na Canada, Colombia na New Zealand ilhali Kundi C likiwa na Uhispania, Brazil, Japan na Nigeria.

Zambia ilishiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza kabisa mnamo 2021 michezo hiyo ilipofanyika Tokyo, Japan. Ilifuzu baada ya kuzishinda timu zenye uzoefu mkubwa kama Cameroon, Nigeria na Afrika Kusini.