26/06/2019

Mtangazaji wa TV akaangwa kuvaa nguo yenye umbo la uume

MASHIRIKA na PETER MBURU

MSOMAJI wa habari za runinga kutoka Australia amekashifiwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia tabia yake ya kuvalia vazi lenye muundo unaofanana na sehemu ya siri ya wanaume.

Bi Samantha Heathwood, mtangazaji wa kituo cha Channel Nine Tv huko Brisbane alishambuliwa baada ya kuvalia vazi la aina hiyo Jumatano alasiri.

Vita vya mitandaoni vilianzishwa na mtazamaji mmoja ambaye alibaini muundo wa nguo ya mtangazaji huyo wa miaka 36, ambaye alikosoa chaguo la fashoni yake.

Vamizi hilo lilivutia watumizi wengi wa mitandao ya Reddit na Facebook kuchangamkia mjadala huo, wengi waki ‘like’ na kuwaita marafiki zao kushuhudia.

Wengine walisema “hatuwezi kujifanya kuwa tunaona meli ilhali ni wazi.”

Hii si mara ya kwanza kwa jaketi hiyo ya kijani kibichi ambayo imetengenezwa na mshonaji Scanlan Theodore imezua hisia kali.

Nguo ya aina hiyo ilizua mjadala mkali mnamo 2016 wakati msomaji mwingine wa habari alivalia wakati wa kusoma habari.

Wanahabari wengine siku za mbeleni aidha wamewahi kukosolewa kutokana na mavazi yao, japo vamizi la majuzi kwa Bi Heathwood yalionekana kushika moto mkubwa.